Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia aanza kurekodi kipindi cha kutangaza utalii

Rais Samia aanza kurekodi kipindi cha kutangaza utalii

Muktasari:

  • Rais Samia ameanza kurekodi kipindi maarufu cha ‘Royal Tour’ chenye lengo la kuitanga Tanzania kimataifa kupitia vivutio vya utalii.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amenza kurekodi kipindi maarufu cha ‘Royal Tour’ chenye lengo la kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia vivutio vya utalii.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 29, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Jaffar Haniu imesema, Rais Samia atatembelea na kuonesha kwa wageni hao vivutio mbalimbali vya utalii, uwekezaji, sanaa na utamaduni vilivyopo nchini.

Taarifa hiyo inayomnukuu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utramaduni, Wasanii na Michezo, Dk Hassan Abbas, imesema Rais Samia na wageni wa Royal Tour wameanza kazi ya kurekodi maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii na uwekezaji Agosti 28/2021 katika maeneo ya visiwa vya Zanzibar.