Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Magufuli ateua ‘wapinzani’ kuwa wakuu wa wilaya, Jokate aenda Kisarawe

Muktasari:

Walioteuliwa ni pamoja David Kafulila aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali (Kasulu Mjini, NCCR Mageuzi), na Patrobas Katambi (aliyekuwa mwenyekiti Baraza la Vijana la Chadema, wote wakiwa wamejiunga na CCM kati ya mwaka jana na mwaka huu.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amefanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa, wilaya, makatibu tawala, makatibu wakuu na manaibu wao, akiteua wanasiasa waliotokea vyama vya upinzani, mshiriki wa shindano la urembo na makada wa CCM.

Rais alitangaza mabadiliko hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam.

Walioteuliwa ni pamoja David Kafulila aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali (Kasulu Mjini, NCCR Mageuzi), na Patrobas Katambi (aliyekuwa mwenyekiti Baraza la Vijana la Chadema, wote wakiwa wamejiunga na CCM kati ya mwaka jana na mwaka huu.

Katambi amekuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma, wakati Machali anaenda Nanyumbu na Kafulila ambaye anakuwa katibu tawala wa mkoa Songwe.

Kadhalika, mrembo aliyeshika nafasi ya pili katika shindano la mlimbwende wa Tanzania (Miss Tanzania 2006), Jokate Mwegelo aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe.

Jokate amechukua nafasi hiyo ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kuondolewa kwenye nafasi ya kaimu katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)

Katika mabadiliko hayo, kada maarufu wa CCM na mwanahabari wa zamani, Jerry Muro ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru.

Muro pia aliwahi kuwa msemaji wa klabu ya Yanga.

Rais pia ametumia mabadilkiko hayo kupandisha vyeo baadhi ya wakuu wa wilaya kutokana na waliokuwa wakuu wa mikoa kustaafu au kuhamishiwa mikoa mingine.

Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa.

Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Albert Chalamila ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya akichukua nafasi ya Amosi Makala aliyehamishiwa Katavi.

Luteni Mstaafu Chiku Galawa, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, amestaafu na nafasi yake kuchukuliwa na Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela.

Wengine ni Brigedia Jenerali, Marco Gaguti aliyekuwa wilaya ya Kibondo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Wengine walioteuliwa katika nafasi za ukuu wa wilaya ni Zainab Kawawa anayeenda Bagamoyo), Said Mkumba (Bukombwe), Mwanahamis Mkunda (Bahi), Sara Msafiri (Kigamboni), Patric Songea (Chato), Cornell Banange (Kasulu) na Joseph Mkilikiti (Hanang’).

Wengine ni Elizabeth Kitundu (Babati), Mary Mahundi (Chunya) Hashim Mgandilwa (Ruangwa), Frank Mwaisungo (Longido) na Ngolo Malinya (Ulanga).

Daniel Chongolo amehamishwa kutoka Longido kwenda Kinondoni).

Katika nafasi za makatibu tawala, walioteuliwa ni Kessy Maduka (Dodoma), Abubakar Kinenge (Dar), Hapiness William (Iringa), Abdallah Malela (Katavi), Rashid Chata (Kigoma), Rehema Madenge (Lindi) na Theresia Mbando (Pwani).

Kwa upande wa Makatibu wakuu Rais Magufuli alimteua Profesa Elisante ole Gabriel kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Mifugo. Awali, alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Profesa Joseph Buchiweshaija amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji.