Rais Kenyatta akutana na Ruto

Rais mteule wa Kenya, William Ruto amekutana na Rais anayemaliza muda wake, Uhuru Kenyatta Ikulu ikiwa ni siku moja kabla ya Ruto kuapishwa kuliongoza taifa hilo.
Muktasari:
- Rais mteule wa Kenya, William Ruto amekutana na Rais anayemaliza muda wake, Uhuru Kenyatta Ikulu ikiwa ni siku moja kabla ya Ruto kuapishwa kuliongoza taifa hilo.
Nairobi. Rais mteule wa Kenya, William Ruto amekutana na Rais anayemaliza muda wake, Uhuru Kenyatta Ikulu ikiwa ni siku moja kabla ya Ruto kuapishwa kuliongoza taifa hilo.
Wawili hao wamekutana leo Jumatatu Septemba 12, 2022 baada ya miezi kupita ambapo wiki iliyopita Ruto alisema wana miezi sasa hawajazungumnza.
Rais Kenyatta anatarajiwa kukabidhi madaraka rasmi kesho ambapo Rais mteule Ruto ataapishwa.
Hafla ya uapisho ambayo itafanyika katika uwanja wa MISC Kasarani inatarajiwa kuhudhuriwa na Marais 20 kutoka Afrika.
Marais wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakiwamo Samia Suluhu Hassan (Tanzania), Yoweri Museveni (Ugaanda), Paul Kagame (Rwanda), Évariste Ndayishimiye (Burundi) na Salva Kiir wa South Sudan.
Pamoja na Marais, viongozi mbalimbali watakaohudhuria, Wakenya 60,000 wanatarajiwa kuingia katika uwanja huo wa Kasarani kushuhudia Ruto na Naibu wake, Rigathi Gachagua wakila kiapo.
Taarifa kutoka katika uwanja huo zinasema kuwa, maandalizi yanaendelea vizuri huku majeshi yakifanya mazoezi kujiandaa kwa siku hiyo muhimu.