Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Radi yaua wanafunzi saba, yajeruhi 82 wakiwa darasani Geita

Muktasari:

  • Mvua kubwa iliyoambatana na radi iliyonyesha wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita, imesababisha vifo vya wanafunzi saba na kujeruhi 82 wa Shule ya Sekondari Businda. Majeruhi wanaendelea na matibabu hospitalini.

Geita. Wanafunzi saba wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Businda, iliyopo wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita, wamefariki dunia na wengine 82 kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi wakiwa darasani.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Paskas Muragili, akizungumza na Mwananchi, amesema tukio hilo limetokea leo Jumatatu, Januari 27, 2025, akieleza kuwa miongoni mwa majeruhi 82, wawili wana hali mbaya.

Mkuu wa wilaya Bukombe, Paskas Muragili akiwajulia hali wanafunzi wa shule ya Sekondari Businda waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Bukombe kwa matibabu baada ya kupigwa na radi wakati wakiwa darasani.

“Wakiwa darasani wakati mvua inanyesha, ilipiga radi na saba wamepoteza maisha. Kwa muonekano, sita ni wavulana na mmoja ni msichana, lakini bado tunafuatilia kujua majina yao kwani mimi sijaingia kwenye mochwari.

""Bado hatujawatambua waliopoteza maisha, lakini baadhi ya majeruhi tayari wameongea na kutuambia majina yao. Kadri hali inavyoendelea, tutapata taarifa rasmi," ameongeza.

Mkuu huyo wa wilaya amesema kwamba, baada ya tukio hilo, madaktari walifika haraka shuleni hapo.

Hilo ni tukio la tatu kutokea mkoani Geita. Oktoba 18, 2019, wanafunzi 39 wa Shule ya Msingi Ihumilo, wilayani Geita, walijeruhiwa kwa kupigwa na radi, na Oktoba 17, 2018, wanafunzi sita wa Shule ya Msingi Emaco Vision walifariki dunia na wengine 23 kujeruhiwa kwa kupigwa na radi wakiwa darasani.


Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi.