Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

QNET yafafanua na kulaani matumizi mabaya ya Jina Lake

Dar es Salaam. Kampuni ya QNET inayojihusisha na mauzo ya moja kwa moja inayolenga ustawi na mtindo wa maisha ulio bora imelani matumizi mabaya ya jina lake katika kisa cha kukamatwa kwa vijana 50 mkoani Tanga kwa kuwalaghai watu mtandaoni.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, baadhi ya watu walidaiwa kudanganywa na kuaminishwa kuwa wangelipwa mshahara wa Sh450,000 kwa mwezi kupitia biashara hiyo, lakini badala yake walijikuta wakiishi katika mazingira mabaya yaliyosongamana bila kipato walichoahidiwa.

“Kufuatia hatua hiyo QNET inachukua fursa hii kufafanua kuwa haihusiki na shughuli hizi za kikatili na inalaani vikali matumizi mabaya ya jina lake na wahalifu waliojitambulisha kuwa ni wawakilishi wa kampuni hiyo,” inaeleza taarifa yao kwa umma.

QNET ni kampuni maarufu ya mtindo wa maisha na ustawi inayotumia mfano wa biashara wa mauzo ya moja kwa moja kutoa bidhaa nyingi za kipekee zinazowezesha watu kuishi maisha yenye afya na uwiano.

QNET inatoa bidhaa zake duniani kote kupitia portal yake ya e-commerce. Wateja wengi huchagua kuwa wasambazaji wa bidhaa hizi kwa kujisajili kama wawakilishi huru, wakipata kamisheni kwa bidhaa wanazouza.

Kampuni hiyo imehimisha vyombo vya habari na mamlaka kutambua tofauti kati ya QNET, kampuni halali ya mauzo ya moja kwa moja, na vyombo au watu wowote wanaotumia jina lake kwa madhumuni ya udanganyifu.

“QNET inabaki kujitolea kudumisha viwango vya juu zaidi vya uadilifu na uwazi katika shughuli zake zote za kibiashara na itaendelea kushirikiana kikamilifu na mamlaka kulinda chapa na wateja wake dhidi ya aina yoyote ya udanganyifu au ulaghai”

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa QNET pia imeanzisha namba ya mawasiliano kwa ajili ya kupokea ripoti za shughuli za ulaghai. Kampuni inahimiza umma kuripoti shughuli yoyote ya kutiliwa shaka inayofanyika kwa jina la QNET kwa namba ya WhatsApp, +233256630005 au kupitia barua pepe kwa [email protected].

Tangu kuanza kwa biashara yake 1998, Bidhaa maarufu zinazotolewa na QNET ni pamoja na saa za kifahari na vito vya Bernhard H. Mayer, bidhaa za utunzaji wa nyumbani za HomePure na nyingine nyingi.