Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Puma Energy yaunga mkono mapinduzi ya nishati safi

Muktasari:

  • Mchango wa sekta binafsi katika kuunga mkono jitihada za serikali unaendelea kudhihirisha kuwa mafanikio ya taifa ni matokeo ya mshikamano wa pamoja.

Dodoma. Katika kuunga mkono jitihada za serikali kampeni ya nishati safi ya kupikia kwa Watanzania, kampuni ya Puma Energy Tanzania imejitokeza kuunga mkono maadhimisho ya Siku ya Samia kwa kutoa msaada wa mitungi ya gesi kwa wakazi wa Dodoma.

Msaada huo umetolewa leo Juni 3, 2025 katika hafla ya kitaifa ya maadhimisho hayo, ambapo kampuni hiyo ilikabidhi mitungi ya gesi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, ikiwa ni ishara ya ushirikiano wa karibu kati ya sekta binafsi na serikali katika kuendeleza matumizi ya nishati safi nchini.

Akizungumza wakati wa tukio hilo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya Nishati Safi, Jeffrey Nasser amesema wanaunga mkono ajenda ya taifa ya nishati safi kikamilifu.

“Puma Energy inaunga mkono kikamilifu ajenda ya taifa ya kuhakikisha kila kaya inapata fursa ya kutumia nishati salama na rafiki kwa mazingira. Hili ni eneo ambalo Rais wetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ameweka msisitizo mkubwa,” amesema.

Tangu mwaka 2024, serikali kupitia kampeni za kuhamasisha matumizi ya gesi kwa kupikia, imefanikiwa kuongeza matumizi hayo kutoka asilimia 6 hadi 16 kwa kipindi cha mwaka mmoja, mafanikio ambayo Puma Energy imeeleza kuwa yanaonesha dhamira ya dhati ya kuwalinda Watanzania dhidi ya madhara ya nishati chafu kama mkaa na kuni.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ameishukuru kampuni hiyo kwa kujitokeza kuunga mkono maono ya serikali, akisisitiza kuwa mchango huo si wa kupuuzwa.

“Tunatambua na kuthamini ushirikiano kutoka kwa wadau kama Puma Energy ambao wamekuwa bega kwa bega na serikali katika kutekeleza sera za nishati safi. Tunawakaribisha wengine kuiga mfano huu,” amesema RC Senyamule.

Hatua hiyo ya Puma Energy imeelezwa kuwa ni sehemu ya mwendelezo wa jitihada zake za kuhakikisha bidhaa za Puma Gas, zilizozinduliwa mwaka 2022, zinafikia Watanzania wengi kwa gharama nafuu na usalama wa hali ya juu.