Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Profesa Mkenda ataka elimu ya amali shule binafsi

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda

Muktasari:

  • Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amekutana na wamiliki wa shule binafsi nchini na kujadili changamoto zinazowabili kwenye sekta hiyo.

Dodoma. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amewaomba wamiliki wa shule binafsi nchini kutoa elimu ya amali ambayo mtalaa wake utaanza kutumika Januari 2024.

Profesa Mkenda ametoa ombi hilo leo Jumanne Oktoba 10, 2023 kwenye mkutano wake na wamiliki wa shule binafsi za msingi na sekondari nchini.

Amesema maandalizi ya mitaala hiyo ipo tayari na kwa sasa iko kwenye maboresho ya mwisho ambapo kama yatapitishwa kama yalivyo mtaala huo utaanza kutumika Januari mwaka 2024.

Amesema ni wakati sasa wa shule binafsi kuanza kutoa mafunzo ya elimu ya amali ambapo katika kutekeleza hayo serikali itaboresha miundombinu kwa shule ambazo zitakuwa tayari kutoa elimu hiyo.

Profesa Mkenda amesema lengo la Serikali ni kutaka kutoa elimu bora kwa wanafunzi ambapo watakapomaliza wawe na ujuzi wa kujiajiri na kuajiriwa hivyo sekta binafsi kama wadau wajitokeze kwa ajili ya kutimiza lengo hilo la serikali.

“Kwenye elimu hii ya amali tutakuwa na michezo, kilimo pamoja na ufundi ambapo mtoto atakapomaliza kusoma atapata na cheti chake alichosomea hivyo nawaomba kama kuna mtu ana uwezo wa kutoa elimu hii awasiliane na serikali na sisi tutaboresha mazingira yake,” amesema Profesa Mkenda.

Amesema shule zote ambazo zinataka kutoa elimu ya amali ni lazima ziwe zimeandaa mazingira mazuri kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na vifaa vya michezo, kilimo pamoja na ufundi stadi ili kuwawezesha wanafunzi hao kupata ujuzi unaotakiwa.

Aidha amezipongeza shule binafsi nchini kwa kuwa na mazingira bora ya kufundishia ambayo ayamepelekea serikali sasa kuboresha mazingira ya shule za umma ili yaendane na shule binafsi.

Amesema kwa kiwango kikubwa sasa Watanzania wameacha kuwapeleka watoto wao kusoma nje ya nchi kwani elimu wanayoipata nchini imeboreshwa kutokana na uwepo wa shule binafsi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi amewataka wamiliki hao wa shule binafsi kuzingatia maadili wakati wa kutoa elimu ili wazalishe vijana watakaokuja kuwa viongozi bora hapo baadaye.

Katambi amesema hakuna haja ya kufaulisha watoto wote lakini hawana maadili na baadaye wanakuwa mzigo kwa Taifa bali wazingatie maadili wakati wa kutoa elimu nchini.

Naye mmiliki wa shule ye St Gasper, Sister Aurelia Kyara amesema kikao hicho ni muhimu kwao kwani ni cha kwanza kufanywa na serikali kwa kuwakutanisha na wamiliki wa shule binafsi kwa ajili ya kujadili changamoto zinazowakabili.