Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi wazingira kanisa la Askofu Gwajima

Muktasari:

  • Jana Jumanne, Serikali ya Tanzania, ilitangaza kulifuta Kanisa la Uzima na Ufufuo linalomililiwa na Askofu Jasephat Gwajima kwa sababu limekiuka taratibu za kisheria za uchaguzi.

Dar es Salaam. Ni ulinzi eneo lote! Ndiyo hali halisi ilivyo kwenye Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima, Ubungo Dar es Salaam.

Kanisa hilo limezungushwa utepe wa njano wenye maandishi meusi huku askari polisi zaidi ya 20 wakiwa wamelizunguka kuimarisha ulinzi.

Askari hao wenye silaha wametanda katika maeneo mbalimbali kuzunguka kanisa hilo ambalo limefutwa.

Uamuzi wa kufutwa umetangazwa jana Jumatatu, Juni 2, 2025 na Serikali ukisema mahubiri ya Askofu Gwajima yamekiuka taratibu za usajili.

Barua ya kututwa kwa kanisa hilo ambayo ilitumwa kwa Askofu Gwajima, nakala ilitumwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Camillus Wambura.

Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima lililopo Ubungo Dar es Salaam wakiwa wamekaa nje ya kanisa hilo baada ya kanisa lao kufutwa Juni 3, 2025.



Mwananchi iliyo jirani na kanisa hilo, leo Jumanne, Juni 3, 2025 limeshuhudia defenda zaidi ya sita za polisi zikiwa na askari wa kutuliza ghasia wakiimarisha ulinzi.

Nje ya lango kuu la kanisa pia kuna gari ya maji ya kuwasha ambayo imepaki kusubiri lolote, huku ndani ya eneo lililozungushwa utepe kukiwa na magari binafsi ambayo yamekumbwa na kadhia hiyo ya utepe.

Upande wa pili wa barabara baadhi ya watu wanaodhaniwa wengine ni waumini wa kanisa hilo wamekusanyika wakiangalia namna kanisa lao lilivyozingirwa na polisi.

Usiku wa jana, Askofu Gwajima alisema kuna polisi wamefika kanisani hapo na hakujua sababu huku akisema hakuna wa kulifunga kanisa la Mungu.


Taarifa zaidi endelea kufuatilia Mwananchi