Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi waimarisha ulinzi kunapofanyika mkutano mkuu Chadema

Gari la askari wa kutuliza ghasia (FFU) likiwa nje ya nje ya mageti ya kuingia Mlimani City panapofanyika mkutano mkuu wa Chadema leo Jumanne Januari 21, 2025.

Muktasari:

  • Wajumbe wa mkutano huo leo Januari 21, 2025 wanatarajia kuchagua mwenyekiti wa chama na makamu wenyeviti wa Bara na Zanzibar, ambapo ushindani mkali upo kati ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Makamu wake, Tundu Lissu wanaogombea uenyekiti.

Dar es Salaam. Zikiwa zimebaki saa chache kuanza kwa mkutano mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), tayari polisi wametanda kwenye eneo la Mlimani City kunapofanyika mkutano huo.

Wajumbe wa mkutano huo leo Januari 21, 2025 wanatarajia kuchagua mwenyekiti wa chama na makamu wenyeviti wa Bara na Zanzibar, ambapo ushindani mkali upo kati ya Mwenyekiti wa chama icho, Freeman Mbowe na Makamu wake, Tundu Lissu wanaogombea uenyekiti.

Mwandishi wa Mwananchi aliyepiga kambi eneo hilo ameshuhudia magari manne ya polisi yakiwa na askari wa kutuliza ghasia (FFU) zaidi ya watano kwa kila gari nje ya mageti ya kuingia Mlimani City asubuhi hii.

Gari la askari wa kutuliza ghasia (FFU) likiwa nje ya nje ya mageti ya kuingia Mlimani City panapofanyika mkutano mkuu wa Chadema leo Jumanne Januari 21, 2025.


Hali ilivyo ukumbini

Katika ukumbi wa Mlimani City, maandalizi yanaendelea ukiwamo ubandikaji wa mabango mengine yakiwa na picha za wagombea na mengine ya Chadema ambayo yana kaulimbiu ya, 'Stronger Together' na mengine yakiandikwa miaka 30 ya Chadema (hata hivyo mwaka huu inatimiza miaka 32 tangu ilipopata usajili wa kudumu mwaka 1993 baada ya kuasisiwa 1992).

Katika hali hiyo ya utulivu, watu wanaendelea kusogea katika eneo hilo, huku shughuli za usafi nazo zikiendelea ndani na nje ya ukumbi huo na wengine wakiwa nje ya ukumbi wakiendelea na upishi.

Mbali na polisi waliopo nje ya geti, ndani ya mageti kuna askari wa kampuni ya ulinzi wakiendelea kuimarisha usalama.

Mkutano mkuu wa Chadema unatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa, ukienda sanjari na uchaguzi wao wa kupata mwenyekiti na makamu mwenyekiti.

Mbali na Mbowe na Tundu Lissu, mgombea mwingine anayewania uenyekiti ni Charles Odero.

Kwenye nafasi ya makamu mwenyekiti Bara, wanaochuana ni Ezekia Wenje, John Heche na Mathayo Gekul.

Kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar, wanaochuana ni Hafidh Ali Saleh, Said Issa Mohammed, Said Mzee Said na Suleiman Makame Issa.