Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni siku ya kuzaliwa, uamuzi kwa Chadema

Muktasari:

  • Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo Januari 21, 2025 kinatimiza mwaka wa 32 tangu kisajiliwe.

Dar es Salaam. Ilianza siku, mwezi, mwaka, muongo na sasa ni miongo mitatu, Happy birthday Chadema.

Happy birthday Chadema katika siku ya uamuzi ama wa kuionyesha Dunia ukomavu wako, au kujielekeza kibra tayari kwa kifo.

Kwa miaka 32 umeuvuka uchanga, utoto, ujana na sasa u mtu mzima, viwalo vya sikukuu si stahiki yako.

Ama Charles Odero, Freeman Mbowe au Tundu Lissu ni hiari yako, umoja na mshikamano baada ya kuwachagua, utaiweka Dunia karibu nawe sako kwa bako.

Unaweza ukavuka kama unavyojinasibu na 'Stronger Together' kwa upande mmoja, lakini kadri utakavyohemka utakuta umetwezwa.

Leo, Januari 21, 2025 Chadema inatimiza miaka 32 tangu ilipopata usajili wa kudumu mwaka 1993 baada ya kuasisiwa 1992.

Lakini, leo chama hicho kinafanya mkutano mkuu wa uchaguzi utakaomaliza ubishi wa nani kati ya Lissu, Mbowe na Odero atakayekuwa mwenyekiti kwa miaka mitano ijayo.

Ni uchaguzi ulioteka hisia kutokana na nguvu na ushawishi ndani ya chama hicho, walionao washindani wawili katika nafasi ya uenyekiti, Mbowe na Lissu.

Pengine ndio uchaguzi utakaothibitisha kweli wa mafahari wawili hawalali zizi moja, au sauti moja haitungi wimbo.

Sambamba na nafasi za uenyekiti, Makamu Mwenyekiti Bara na Zanzibar wanatarajiwa kupatikana katika uchaguzi huo utakaofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Wanaogombea nafasi ya makamu mwenyekiti bara ni John Heche, Ezekia Wenje na Mathayo Gekul.

Kwa upande wa makamu mwenyekiti Zanzibar, ni Hafidh Ali Saleh, Said Issa Mohammed, Said Mzee Said na Suleiman Makame Issa.

Minyukano na matumaini ya ushindi yameendelea kuonekana kwa kila upande katika mitandao ya kijamii.