Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi mbaroni akidaiwa kusafirisha mirungi

Askari Polisi wa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha, Sajenti Ismael Katenya (48), akiwa chini ya ulinzi wa polisi wilayani Mbulu mkoani Manyara, akidaiwa kukutwa anasafirisha bunda 340 za dawa za kulevya aina ya mirungi.

Muktasari:

  • Polisi mkoani Manyara, inamshikilia askari wa jeshi hilo  wa kituo kikuu cha Polisi Arusha akidaiwa kukutwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi

Mbulu. Askari wa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha, Sajenti Ismael Katenya (48), anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Manyara, akidaiwa kukutwa akisafirisha bunda 340 za dawa za kulevya aina ya mirungi.

Inadaiwa kuwa Katenya alikuwa anasafirisha bunda hizo 340 zinazokadiriwa kuwa ni kilo 140 alizozifunga kwenye magunia manne akitoka Arusha akielekea mkoani Mara.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi (ACP), George Katabazi akizungumza leo Januari 22, 2024  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kamanda Katabazi amesema askari  huyo alikamatwa Januari 22, 2024 saa 9 alasiri katika Mtaa wa Silaloda Tarafa ya Endagikot wilayani Mbulu.

Amesema Polisi huyo anadaiwa alikuwa anasafirisha dawa hizo za kulevya kwenye gari aina  ya Nissan Patrol station wagon.

Amedai kuwa polisi huyo alifunga dawa hizo ndani ya magunia manne ambapo kila gunia moja alipakia bunda 50, bunda 40 zilikuwa ndani ya mfuko wa salfeti, bunda 87 zilikuwa kwenye begi jeusi kubwa na bunda 53 ndani ya begi dogo jeusi.

"Alipakia dawa hizo za kulevya ndani ya gari na kusafirisha kama mizigo  ndipo akakamtwa na askari waliokuwa doria," amesema Kamanda Katabazi.

Mmoja kati ya shuhuda wa tukio hilo, Abdilahi Bayo amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kumkamata bila kujali ni askari mwenzao.