Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi kufanya uchunguzi mwanakijiji kuuawa, kutupwa kisimani

Kaimu Kamanda wa Polisi Mtwara, Isack Mushi akiongea na waandishi wa habari leo. Picha na Florence Sanawa

Muktasari:

  • Mtu mmoja mkazi wa Kijiji cha Mngoji amekutwa amefariki dunia baada ya kushambuliwa ma watu wasiojulikana katika sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo kichwani hali ambayo ilisababisha kupoteza damu nyingi hivyo kusababisha kifo chake.

Mtwara. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linaendelea kufanya uchunguzi wa tukio la mauaji ya Abdul Abdulmajid (47) mkazi wa Kijiji cha Mngoji, Kata ya Madimba ambaye alikutwa akiwa amefariki dunia baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani na watu wasiofahamika, huku mwili wake ukitupwa jirani na kisima.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polisi, Isack Mushi alisema kuwa Februari 17 majira ya saa nane mchana katika Kata ya Madimba wananchi walibaini kuwepo kwa tukio la mauaji.

Amesema kuwa uchunguzi wa kitabibu uliofanywa na daktari ulibaini kuwa chanzo cha kifo hicho ni kuvuja damu nyingi kutokana na jeraha alilokuwa nalo kichwani hata hivyo sababu ya tukio hilo bado inachunguzwa.

"Juhudi za kuwasaka watu waliohusika na tukio hilo zinaendelea Ili kuweza kuwafikisha mbele ya Sheria na Jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua waharifu wote watakaobainika kujihudisha na vitendo kama hivi," alisema Mushi.

"Pia elimu inaendelea kutolewa kwa jamii Ili kuchat kujichukulia sheria mikononi ili kuhakikisha kuwa vitendo vya kiharifu  vinavyogharimu maisha ya watu vinakomeshwa," alisema Mushi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mngoji, Issa Nampalangula alisema kuwa tukio hilo limezua taharuki kijijini hapo kwakuwa marehemu hakuwa na ugomvi na mtu.

"Ni kweli tulipata taarifa ya mwananchi kujeruhiwa tulifika eneo la tukio ambapo alikuwa anapatiwa huduma ya kwanza baada ya kutolewa kando ya kisima  ilibainija alikuwa amejeruhiwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake na alikuwa hajitambui na akiwa amejeruhiwa vibaya hali ambayo ilitishia amani hapa kijijini," alisema Nampalangula.