Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi Dar warushiana mpira mkutano Chadema

Muktasari:

  • Chadema kwa kushirikiana na wadau na Taasisi mbalimbali, kufanya mkutano wa hadhara kujadili mkataba wa bandari Julai 23.

Dar es Salaam. Polisi Dar es Salaam wamerushiana mpira kuhusu mkutano wa hadhara  Chadema, Kanda ya Pwani uliopangwa kufanyika Jumapili Julai 23,2023 wenye ajenda ya mkataba wa bandari.

Mkutano huo utakaofanyika viwanja vya Bulyaga, Temeke unatarajiwa kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwemo viongozi wa dini, wanasiasa na wanasheria.

Hata hivyo, wakati Chadema leo Ijumaa Julai 21, 2023 wakitangaza kufanya mkutano huo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro hajaweka wazi kama wametoa kibali au la.

Kamanda Muliro Jumanne amesema, “Sala la mikutano ya vyama vya siasa wanaohusika na makamanda wa polisi wa wilaya. Kisha akakata simu.

Hata hivyo, Mwananchi lilipomtafuta Kamanda wa Polisi wa Temeke, Kungu Malulu alidai yeye sio msemaji badala yake atafutwe Kamanda wa Muliro.

Taarifa ya mkutano huo imetolewa, wakati mjadala wa mkataba wa uwekezaji bandari baina ya Tanzania na kampuni ya DP World ukiendelea kushika kasi katika maeneo mbalimbali.

Akizungumza na wanahabari Kaimu Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Baraka Mwago amesema mkutano huo utahudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwemo viongozi wa dini wanasheria na watu wegine kutoka taasisi na makundi maalumu.

"Chadema katika suala la bandari tumeamua kutofanya siasa. Tumeamua kushirikisha watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wanasheria, na wadau kutoka taasisi nyingine,” amesema Mwago.