PIRAMIDI YA AFYA: Magonjwa yanayoenezwa na wanyama kwa binadamu

Muktasari:
Baada ya timu iliyoundwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya kubaini kuwa wagonjwa waliougua ugonjwa usiofahamika kusini mwa Tanzania wilayani Ruangwa, Mkoa wa Lindi ni homa ya mgunda ambao kitabibu hujulikana kama Leptospirosis, leo nitawapa ufahamu wa ugonjwa huu pamoja na magonjwa mengine ambayo mara kwa mara yanawapata watu ambayo yanatoka kwa wanyama kwenda kwa binamu.
Baada ya timu iliyoundwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya kubaini kuwa wagonjwa waliougua ugonjwa usiofahamika kusini mwa Tanzania wilayani Ruangwa, Mkoa wa Lindi ni homa ya mgunda ambao kitabibu hujulikana kama Leptospirosis, leo nitawapa ufahamu wa ugonjwa huu pamoja na magonjwa mengine ambayo mara kwa mara yanawapata watu ambayo yanatoka kwa wanyama kwenda kwa binamu.
Mtakumbuka tangu ugonjwa huu ulipobainika kusini mwa Tanzania mkoani Lindi ulileta taharuki kutokana na jamii kutowahi kukumbana na dalili na viashiria ambayo si vya ugonjwa unaofahamika.
Ugonjwa huu unazuilika na kutibika, dawa za antibiotic na kutuliza homa na maumivu hutolewa katika matibabu.
Njia kuu za kujikinga ni pamoja na kuepuka kugusa maji au vitu vilivyochafuliwa na mkojo wa wanyama na kunywa maji safi na salama yaliyochemshwa zaidi ya nyuzi joto 50.
Fika mapema katika huduma za afya mara tu anapoona dalili na viashiria pamoja homa, maumivu ya misuli, uchovu wa mwili, mwili kuwa na rangi ya manjano, macho kuvilia damu, kutokwa damu na kukohoa damu. Wafugaji au wale wote wanaoishi jirani na mifugo kuzingatia njia zote za kujikinga.
Kwa mujibu wa kituo cha udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza, katika kila visa 10 vya magonjwa ya kuambukiza vinavyofika katika huduma za afya, sita vitokanavyo na vimelea wanaotoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
Magonjwa haya yanaweza kuingia kwa binadamu kwa njia ya kinywa, ngozi, hewa.
Magonjwa yanayoenea kutoka kwa wanyama kwenda kwa wengine hujulikana kitabibu kama Zoonotic diseases huwa si lazima yamfanye mnyama aumwe, bali kumfanya binadamu awe mgonjwa .
Magonjwa mengine ambayo yanatoka kwa wanyama kuja kwa binadamu ambayo Shirika la Afya Duniani (WHO) wanayapa kipaumbele katika kuyadhibiti ni pamoja na kimeta, bruselosisi, homa ya bonde la Ufa, virusi vya Nile ya magharibi na mafua ya infulenza kama vile ya nguruwe.
Vile vile kichaa cha mbwa, homa ya mapafu jamii ya virusi vya Uviko-19 ikiwamo virusi vya mashabiki ya kati, ugonjwa wa Laimu, salmonela na ugonjwa wa tauni.
Magonjwa haya yanaathari za wastani kwa muda mfupi mpaka mrefu na baadhi huweza kusababisha kifo kama hatua za matibabu zisipochukuliwa.
Njia za kiujumla za kujikinga na magonjwa haya ni pamoja na kuepuka kugusana kimwili na wanyama hasa wanaoneka kuugua, kuepuka kugusana na maji maji ya mwilini ya wanyama ikiwamo mate, kamasi na damu.
Kwa wale wanaoishi na jirani na wanyama wanaofugwa majumbani kuhakikisha wanapatiwa chanjo na kuzingatia ushauri wa madaktari wa mifugo na tiba.
Kutoa taarifa mapema kwa mamlaka husika kwa wanyama kama mbwa ambao wataonyesha dalili za kushambulia watu.