Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Padri Ngowi wa Shirika la Damu Aziz ya Yesu afariki dunia kwa ajali

Padri Nicolaus Ngowi enzi za uhai wake

Dodoma. Padri Nicolaus Ngowi wa Shirika la Damu Aziz ya Yesu Tanzania amefariki dunia jana Jumatatu Septemba 9, 2024 kwa ajali ya gari alipokuwa safarini kuelekea nyumbani kwao Marangu, mkoani Kilimanjaro katika shughuli ya familia.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mkuu wa Shirika hilo, Vedasto Ngowi akisema padri huyo alikuwa akielekea nyumbani kwao Marangu mkoani Kilimanjaro.

“Sijajua alikuwa anaelekea katika shughuli gani lakini alikuwa apokewe na ndugu zake njia panda (Himo), hivi sasa tunaelekea nyumbani kwake Marangu,”amesema Ngowi.

Amesema taratibu zaidi zitajulikana baada ya kuwasiliana na familia yake lakini mazishi yatafanyika Manyoni mkoani Singida.

Endelea kufuatilia mitandao ya Mwananchi kwa taarifa zaidi