Padri Medard Weyemere afariki dunia

Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Desderius Rwoma
Muktasari:
Askofu Rwoma asema mazishi ya padri huyo yatafanyika kesho Jumatano katika makaburi ya mapadri wa jimbo hilo yaliyopo katika Seminari ya Rubya.
Dar es Salaam. Aliyewahi kuwa Mkuu wa Seminari za Rutabo na Rubya mkoani Kagera, Padri Medard Weyemere, amefariki dunia.
Katika tangazo la kifo hicho, Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Desderius Rwoma amesema kifo hicho kimetokea jana Aprili 2, 2018 katika Hospitali ya Rufaa Bugando.
Askofu Rwoma amesema mazishi ya padri huyo yatafanyika kesho Jumatano katika makaburi ya mapadri wa jimbo hilo yaliyopo katika Seminari ya Rubya.