Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ongezeko la wanafunzi nchini haliendani na walimu

Wanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Kambarage Halmshauri ya Mji wa Kibaha Mkoani Pwani wakiwa darasani Januari 9, 2023 waliporipoti shuleni. Picha na maktaba.

Muktasari:

  • Ongezeko la wanafunzi limechagizwa kwa hatua zaidi na sera ya elimu bila malipo, ambapo kabla ya mwaka 2016 kulikuwa na ushirika wa malipo kati ya wazazi na Serikali.

Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa kasi ya ongezeko la wanafunzi nchini haiendani na kasi ya ongezeko la walimu na madarasa ambavyo ni vichocheo muhimu vinavyosaidia upatikanaji wa elimu bora.

 Hayo yameelezwa na Mhariri wa Takwimu gazeti la Mwananchi, Halili Letea pamoja na Mwandishi mbobezi wa habari za elimu gazeti la The Citizen, Jacob Mosenda walipokuwa wakichokoza mada katika mjadala wa Mwananchi Twitter Space leo Jumatano Januari 11, 2023.

Mjadala huo unajadili kipi kifanyike ongezeko la uandikishaji darasa la kwanza na kidato cha kwanza, liendane na utoaji wa elimu bora nchini.

“Uwiano wa wanafunzi na walimu hauendani, kwa kipindi cha mwaka 2016 uwiano wa walimu kwa wanafunzi ilikuwa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 42 mpaka mwaka 2022 ilikuwa wanafunzi 65 katika shule za umma nah ii ni kwa mujibu wa takwimu za Tamisemi.

“Baadhi ya wilaya kuna uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 100 suala la madarasa mwaka 2016 uwiano ilikuwa 73 mpaka mwaka 2022 shule za msingi darasa moja lilikuwa  na wanafunzi 81 msongamano wa madarasani umeendelea kuongezeka,” amesema Letea.

Mosenda amesema ongezeko la wanafunzi limechagizwa kwa hatua zaidi na sera ya elimu bila malipo, ambapo kabla ya mwaka 2016 kulikuwa na ushirika kati ya wazazi na Serikali.

“Mwaka 2016 sera mpya ilianza kutekelezwa jukumu la wazazi likahamia kwa Serikali ambayo imebeba jukumu zima la watoto wanaotakiwa kuingia darasa la kwanza mpaka kidato cha tano, wazazi wengine sasa wamebweteka, tunapozungumzia ubora wa elimu uhusika mkubwa wa wazazi unawafanya kuona ni jukumu la Serikali,” amesema.

Amesema licha ya baadhi ya miundombinu kuboreshwa ikiwemo ujenzi wa madarasa bado kuna changamoto ya rasilimali watu.

“Uwepo wa miundombinu ya kutosha ambayo imejengwa hivi karibuni kutokana na fedha za Uviko imechangia kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi shuleni, hata hivyo kuna changamoto kubwa ya upungufu wa walimu hivyo wachache waliopo wanalazimika kufundisha katika darasa lenye wanafunzi wengi,” amesema.

Mosenda amesema bado kuna changamoto walimu wengi wanaoajiriwa bado wanafika kwa ajili ya kuziba pengo la waliostaafu na siyo kujaza maeneo yenye upungufu.