Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NHIF: Hatujabadilisha huduma Toto Afya Kadi

Muktasari:

  • Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga amesema, tangu walipoboresha Toto Afya Kadi tayari shule zaidi ya 240 zimejiunga na wanapatiwa huduma. 

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga amesema mfuko huo haujabadilisha huduma za kifurushi cha Toto Afya Kadi, bali kilichokifanya ni maboresho ya kifurushi hicho. 

Konga ameyasema hayo leo Septemba 20 alipokuwa akijibu maswali ya wachangia katika mjadala wa X-space iliyoandaliwa na Mwananchi Communications Ltd ikiwa na mjadala wa ‘Mabadiliko ya huduma Toto Afya Kazi nini sababu, matokeo na suluhisho lake?’

Amesema kabla ya maboresho tuliangalia kundi hilo lilikuwa na watoto milioni 26. 

“Tukasema angalau tuwapate asilimia 50 tukatengeneza watoto waliopo mashuleni ni miaka saba na kuendelea tukatengeneza hivyo kuendana na misingi ya bima ya afya ya umma. 

“Waingie wengi zaidi na tuliweka malengo hayo tukiamini kwenye mashule tunaweza kuwapata. Hapo nyuma tulikuwa na watoto 200,000 pekee waliingia kwa hiari lakini wengi waliingia wakiwa wagonjwa,” amesema. 

Amesema tangu walipoboresha Toto Afya Kadi tayari shule zaidi ya 240 zimejiunga na wanapatiwa huduma. 

“Hatujasitisha ilia tunahitaji huduma hii iwe endelevu. Lakini pia watoto ambao walikuwa wanatibiwa na Toto Afya Kadi wanaendelea na matibabu kama kawaida mpaka pale watakapofikia ukomo wa muda wa matumizi ya kadi zao,” amesema. 

Awali akiuliza swali, Mhariri msaidizi wa habari Ibrahim Yamola ametaka kujua utekeloezaji wa sharti la kutaka watoto wafikie 100 ndippo waandikishwe. 
“Kama kulikuwa na lengo zuri kulikuwa na sharti gani kwa shule kuwa na watoto 100? Kuna watoto wanakosa fursa kwakuwa hawajafika watoto 100,” amesema. 

Naye Rukaiya Nasib Msemaji Sekta ya Afya ACT Wazalendo amehoji kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyoonyesha NHIF kupokea Sh5 bilioni lakini wanatumia Sh40.

“Swali la pili bado kama Tanznania tunachangamoto kubwa kwenye mfumo wa kugharamia matibabu kama mfuko wa bima NHIF wamejipangeje?” amehoji.