Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nemc: Uchimbaji madini wahatarisha mazingira Tanzania

Muktasari:

  • Zaidi ya maeneo 1,000 nchini yameharibiwa kutokana na changamoto za uharibifu wa mazingira unaohusisha shughuli za uchimbaji mdogo  hatua iliyoifanya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuanza kazi ya kurejesha maeneo yaliyoharibiwa.

Dar es Salaam. Zaidi ya maeneo 1,000 nchini yameharibiwa kutokana na changamoto za uharibifu wa mazingira unaohusisha shughuli za uchimbaji mdogo wa madini. 

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dk Samuel Gwamaka amesema hali inazidi kuwa mbaya maeneo ya uchimbaji Geita na Chunya mkoani Mbeya.

Uharibifu unaofanyika unahusisha uchimbaji wa mashimo na kuyatelekeza, ukataji wa misitu kwa ajili ya kupanua maeneo ya uchimbaji pamoja na matumizi ya kemikali ya zebaki.

 “Karibu asilimia 30 ya maeneo yote yanayochimbwa Chunya yameharibiwa na hakuna athari zimeanza kuonekana, hakuna uwezekano tena wa maeneo hayo kutumika kwa shughuli za kilimo na vyanzo vya maji vimeharibiwa,”amesema Lumato.

Lumato ametoa kauli hiyo alipozungumza na gazeti hili leo wakati wa Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji na Madini linalofungwa leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Lumato anatoa kauli hiyo wakati mchango wa wachimbaji wadogo ukifikia asilimia 44.3 ya katika masoko ya ndani na nje nchi kwa mwaka 2021/22 na ajira zikiongezeka kupitia leseni za uchimbaji mdogo.

Hatua zilizoanza kuchukuliwa na baraza hilo ni pamoja na pendekezo la kuhamisha mamlaka ya usimamizi wa vyeti vya mazingira kutoka Tume ya Madini na kuwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais.

“Tunataka TMC ipunguzie mzigo huo, lakini pili tumeongeza kanda za NEMC kutoka sita hadi 13 ili kusogea karibu na wadaum lengo ni kushawishi kupunguza uharibifu wa mazingira,” amesema.

Tatu, Lumato amesema baraza hilo limepata ufadhili wa Dola milioni 7.3 za Kimarekani kwa ajili ya kusaidia uchechemuzi wa kupunguza athari za kimazingira.

“Kupitia ufadhili huo, tutakwenda kwenye maeneo baadhi yaliyoathiriwa ili kuyarejesha katika hali yake, hatuwezi kufikia maeneo yote,” amesema.