Ndugu wawili wafariki kwa kupigwa radi wakivua samaki

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha na Florence Sanawa.
Muktasari:
- Ndugu wawili wafariki dunia baada ya kupigwa na radi wakiwa baharini wakivua samaki katika Kata ya Msimbati, mkoani Mtwara.
Mtwara. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limewata wavuvi kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua baada ya wavuvi wawili ndugu kupigwa radi na kusababisha kifo chao Machi 19 katika Kijiji cha Mtandi, Kata ya Msimbati, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema kuwa tukio hilo lilishuhudiwa na wavuvi wenzao waliokuwa wakivua katika eneo hilo.
Katembe aliwataja marehemu hao kuwa ni Shani Salum Yusuph (53) na Nangomwa Salum Yusuph (58) wavuvi wote wakazi wa Kijiji cha Mtandi.
“Siku ya tukio saa 4 asubuhi marehemu hao ambapo ni ndugu walienda baharini wakiwa na mtumbwi ambao haujasajiliwa namba na kuingia baharini kwa lengo la kuvua wakiwa wanavua mvua kubwa ilianza kunyesha ndipo walipopigwa na radi na kufariki ambapo tukio hilo lilishuhudiwa na wavuvi wenzao ambao walitoa taarifa kwa Polisi,” amesema.
“Juhudi zilifanyika na kuwea kuichukua mili ya marahemu na kuiweka ufukweni ambapo kwa mujibu wa majibu ya daktari ilionyesha kuwa vifo hivyo vilitokana na kupigwa radi,” alisema Katembo.