Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndama ahukumiwa kulipa dola 75,000

Ndama ahukumiwa kulipa dola 75,000

Muktasari:

  • Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu mfanyabiashara maarufu nchini,  Ndama Shabani ‘Ndama mtoto wa Ng'ombe’ na mwenzake Yusuph Yusuph kulipa fidia ya dola za kimarekani 75,000 kwa malalamikaji Emanuel Motilhathedi baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu mfanyabiashara maarufu nchini,  Ndama Shabani ‘Ndama mtoto wa Ng'ombe’ na mwenzake Yusuph Yusuph kulipa fidia ya dola za kimarekani 75,000 kwa malalamikaji Emanuel Motilhathedi baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.


Washtakiwa hao wanadaiwa kujipatia dola za kimarekani 150, 000 kutoka kwa mlalamikaji huyo ambaye ni raia wa Botswana kwa madai kuwa wangemuuzia kilo 500 za dhahabu lakini hawakufanya hivyo.


Hukumu hiyo imetolewa leo,  Jumatatu Agosti 2, 2021 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Godfrey Isaya baada ya washtakiwa hao kukiri mashtaka, kupitia majadiliano baina yao na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini ( DPP).