Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nchi za umoja wa ushoroba wa kati sekta ya usafirishaji kukutana Tanzania

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Profesa Goius Kahyarara amesema wizara yake inatarajia kuwa mwenyeji wa kikao cha mawaziri wa sekta ya miundombinu na usafirishaji kutoka nchi za Umoja wa Ushoroba wa Kati.

Nchi hizo ni Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Jumuiya ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC ). 

Profesa Kahyarara amesema zipo nchi zingine mbilli zilizowasilisha maombi ya kujiunga katika ushoroba huo ambazo ni Zambia na Malawi na maombi yao yatawasilishwa katika kikao hicho japo kwa upande wa manaibu makatibu wakuu wao wamekwisharidhia maombi hayo. 

Amesema hayo leo Ijumaa Novemba 3, 2023  alipoitembelea Bandari Kavu ya Kwala iliyopo Mkoa wa Pwani.

Pia, amesema kupitia ziara ya Rais  Samia Suluhu Hassan iliyofanyika hivi karibu nchini Zambia kati ya mambo yaliyoafikiwa kwenye ziara hiyo ni pamoja na kuimarisha umoja wa ushoroba wa kati, reli ya Tazara  na  kuimarisha Bandari ya Dar es Salaam. 

Ameseme lengo kuu la ushoroba ni kuisaidia Bandari ya Dar es Salaam kupata mizigo mingi zaidi pamoja na kuhudumia nchi zinazoizunguka Tanzania hivyo juhudi za kuimarisha Bandari ya Dar es Salaam zinakwenda sambamba na kuimarisha Bandari Kavu ya Kwala.

"Bandari kavu ya Kwala kwa sasa inatoa huduma zote za kibandari kama bandari zingine na kubwa zaidi itarahishia shughuli zinazoendelea Bandari ya Dar Salaam hivyo mteja hatokuwa na haja ya kwenda ofisi za bandari zilizopo Posta jijini Dar es Salaam kwani wanaweza malizia michakato yao yote katika ofisi zilizopo bkBandari Kavu ya Kwala,"  amesema