Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwandishi wa habari afariki dunia kwa uzazi

Marehemu Blandina Aristides enzi za uhai wake

Muktasari:

  • Ni Blandina Aristides ambaye pia Katibu Msaidizi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC), amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa Bugando iliyopo jijini Mwanza alipokwenda kujifungua.

Mwanza. Katibu Msaidizi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC), Blandina Aristides amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko amesema, leo Desemba 26, 2023 kuwa Blandina alifikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya kujifungua na alijifungua kwa upasuaji, lakini hali yake ilibadilika ghafla na kupelekwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) mpaka umauti unamfika.

"Amefariki dunia leo asubuhi pamoja na mtoto wake," amesema Soko na kuongeza kuwa taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika Mabatini laini ya Polisi jijini Mwanza.

 Paulina David, mwandishi wa habari kutoka kampuni la Sahara Media Group ameelezwa kusikitishwa na taarifa za msiba huo.

"Kuna muda hata unashindwa useme nini, pumzika kwa amani Blandina," amesema Paulina.

Naye Albert Sengo, mwandishi mwingine mkoani humo mbali na kusikitishwa na taarifa hiyo, amesema ni wakati sasa wa tasnia hiyo kujitathmini juu ya mchango wao katika kupunguza vifo vya mama na mtoto.

"Nimebaki na maswali mengi. Ila najua Mungu anatukumbusha kitu kwamba bado hatujaitendea haki tasnia yetu hasa linapokuja suala la vifo vya wajawazito na watoto. Kwa nini haya yatokee?" amehoji Sengo.

Mpaka umauti unamfika Blandina alikuwa mwandishi wa habari wa Kampuni la Uhuru Media huku akiwa amehudumu katika nafasi ya Katibu Msaidizi MPC kwa miaka mitatu tangu mwaka 2021.