Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwabukusi ashinda rufaa, sasa kuwania urais TLS

Wakili Boniface Mwabukusi (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Mawakili Vijana kutoka Kutoka Chama Wanasheria Tanganyika (TLS,) Edward Heche wakati wakiwa chumba Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam. Picha na Hadija Jumanne

Dar ES Salaam. Mahakama Kuu imetengua uamuzi wa Kamati ya Rufaa ya TLS uliomwengua Boniface Mwabukusi kwenye kinyang'anyiro cha kugombea urais wa chama hicho cha Wanasheria wa Tanganyika.

Uamuzi huo ambao umetolewa leo Julai 26, 2024 na Jaji Butamo Phillip, ndio unaotoa hatima ya Mwabukusi katika kinyang’anyiro hicho.

Mwabukusi alikuwa mmoja wa wanachama walioomba na kupitishwa na Kamati ya Uchaguzi kugombea nafasi ya urais wa TLS, lakini akapingwa kwenye kamati ya maadili ambayo ilimwengua.

Uchaguzi wa TLS unatarajiwa kufanyika Agosti 2, 2024 jijini Dodoma.


Endelea kufuatilia Mwananchi