Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mvua yakwamisha magari nane ya misiba Kilimanjaro

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu

Muktasari:

  • Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ameeleza namna magari nane yaliyokuwa yamebeba misiba ilivyokwama eneo la Hedaru, wilayani Same kutokana na kukatika kwa mawasiliano ya barabara yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani hapa.

Same. Mvua zinazoendelea kunyesha katika Mkoa wa Kilimanjaro, zimesababisha kukatika kwa mawasiliano eneo la Hedaru, wilayani Same, hali ambayo imesababishwa magari yaliyokuwa yamebaba miili ya marehemu kuja mkoani Kilimanjaro, kushindwa kuendelea na safari.

Changamoto hiyo ilitokea jana usiku, Novemba 23, baada ya mafuriko kusomba mawe na magogo kutoka maeneo ya milimani na kusababisha kuziba kwa barabara kuu ya Moshi - Dar es Salaam na kusababisha magari kushindwa kupita usiku kucha.

Akizungumza leo Ijumaa, Novemba 24  katika mkutano wa waandishi wa habari, Mkuu wa mkoa huo, Nurdin Babu amesema wamefanikiwa kuondoa  mawe  na magogo yaliyokuwa yameziba katikati ya  barabara na kwamba asubuhi magari yalianza kupita.

"Jana mvua kubwa imenyesha maeneo ya milimani kule Same,  imeporomosha mawe na magogo na kuanzia jana saa saba  usiku, hakuna gari ambalo liliweza kupita kuja Moshi, wananchi walikwama eneo hilo,  magari kama nane yaliyokuwa yamebeba misiba kuja kuzika yalishindwa kupita, maiti zilikuwa pale,  kwa hiyo tumekwenda tumeshughulikia tatizo  sasa hivi magari yanapita vizuri,"

"Tulimtuma  Meneja wetu wa Tanroad mkoa amekwenda na mimi na kamati yangu ya usalama tumekwenda kule asubuhi na kazi kubwa na  nzuri imefanyika na magari yanapita bila changamoto yoyote," amesema RC Babu.

Babu amewaomba wananchi wanaoingia mkoani humo kuendelea kuwa watulivu wakati wa changamoto hii ya mvua na kwamba wamepeleka vifaa na wameweza kuondoa magogo na mawe hayo na barabara zinapitika.

Naye, Mkuu wa wilaya hiyo, Kasilda Mgeni amesema kwasasa hali ni shwari na magari yanapita bila changamoto yoyote katika eneo hilo baada ya kufanikiwa kuondoa magogo na mawe hayo ambayo yalitokea maeneo ya milimani kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa sasa.