Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtwara yatajwa biashara ya usafirishaji binadamu

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo akizungumza katika mafunzo ya Usafirishaji wa Binadamu Mtwara. Picha na Florence Sanawa

Muktasari:

  • Mkoa wa Mtwara umetajwa kutokuwa salama katika biashara ya usafirishaji wa binadamu, ambapo wasichana, vijana na watoto wamekuwa wakisafirishwa kwenda katika maeneo mbalimbali ya ndani ya nchi.

Mtwara. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amsema tatizo la usafirishaji wa binadamu ndani ya nchi ni kubwa na Mkoa wa Mtwara hauko.

 Kauli hiyo ameitoa leo Machi 21 katika mafunzo ya usafirishaji wa binadamu yanayotolewa na kwa udhamini wa shirika lilisilo la kiserikali la Hanns Seidel Foundation (HSF) kwa Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji na Ustawi wa jamii.

Amesema kuwa kitendo cha usafafirisha wa binadamu ni haramu na kimekatazwa na sheria za nchi ambazo zina zuia na kupambana na wanaofanya biashara hii.

"Mkoa wa Mtwara hauko salama kwa usafirishaji wa binadamu ambapo baadhi ya mabinti, vijana na watoto wamekuwa wakisafirishwa kwa lengo la kuahidiwa kupatiwa kazi katika hotel za kitalii. Serikali haijakataza watazania kufanyakazi nje ila wameweka sheria za kumlinda Mtanzania," amesema.

Amesema usafirishaji wa binadamu hauna tofauti na utumwa mambo leo, akiihusisha biashara hiyo na soko la ngono linalohitaji wanawake na wasichana na soko la viungo vya binadamu.

“Uhalifu huu hufanyika kwa siri sana waathirika hupata mateso makubwa kupigwa kubakwa kufanyishwakazi bila malipo kunyanganywa hati za kusafiria na wengine kuuwawa.

“Tanzania imekuwa ikitajwa kuwa ni chanzo cha watu kusafirishwa na mapito ya watu wanaopita pia mafikio ya watu wanaoletwa kwa minajili yakutumikishwa bishara hii hufanywa kwa usiri mkubwa," amesema.

Kwa upande wake Edwin Mugambila kutoka shirika lilisilo la kiserikali Tanzania Relief Initiatives (TRI) amesema kuwa jamii iambiwe madhara ya usafirishaji wa binadamu.

"Jamii iambiwe madhara ya usafirishaji wa binadamu ambao umekuwa ukifanyika tumeona tushirikiane na askari Polisi ambao wapo kila kata ili kuweka mikakati ya kuzuia zaidi kuliko kuchukua hatua baada ya tukio kutokea," amesema.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Hanns Seidel Foundation (HSF) Kadele Mahumba alisema kuwa wapo watu wanachukua watoto na kwenda kuwatumikisha kingono ina pelekea biashara hii iendelee kufanyika ‘