Msimamizi wa uchaguzi Kenya atoweka

Muktasari:
- Msimamizi wa uchaguzi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) katika jimbo la Embakasi Mashariki, Daniel Musyoka, ameripotiwa kutoweka.
Msimamizi wa uchaguzi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) katika jimbo la Embakasi Mashariki, Daniel Musyoka, ameripotiwa kutoweka.
Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati ametoa taarifa hizo, jana Ijumaa, Agosti 12 usiku katika ukumbi wa Bomas wakati wa mchakato wa kuhakiki matokeo ya uchaguzi wa Rais.
Chebukati amesema kuwa Musyoka alitoweka Alhamisi Agosti 11, 2022 saa tisa alfajiri katika Shule ya Usafiri ya Anga ya Afrika Mashariki ambako shughuli ya kuhesabu matokeo ya uchaguzi wa urais katika jimbo la Embakasi Mashariki unafanyika.
Hata hivyo, akiwa katika kituo cha kuhesabia kura, aliomba kutoka kwenda kupiga simu lakini hakurudi.
Kesi hiyo iliripotiwa kwa tume ambayo nayo ililitaarifu jeshi la polisi.
“Familia yake inamtafuta lakini haiwezi kumpata,” amesema Chebukati
“Tume ina wasiwasi mkubwa na suala hilo na inahimiza mashirika ya uchunguzi kubaini chanzo cha kutoweka,” mwenyekiti wa IEBC ameongeza.
Nia ya kutoweka kwake ni suala la polisi kuchunguza, lakini Chebukati alihakikisha kwamba kila kitu kiko sawa na kwamba majukumu ya Musyoka yamechukuliwa na naibu wake.
Chini ya Sheria ya Uchaguzi na kanuni zake za wahudumu, Wasimamizi wa Uchaguzi katika majimbo wanapotangazwa kwenye gazeti la serikali kama Wasimamizi wa Uchaguzi wa majimbo (CRO), wanaripoti kwa NRO