Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mshtakiwa wa EPA, aachiwa huru na Mahakama

Johnson Lukaza na mdogo wake Mwesigwa Lukaza wakiwa mahakamani wakisubiri hukumu

Muktasari:

Akitoa  hukumu hiyo  jana Kiongozi wa  jopo la Mahakimu watatu wanaoisikiliza kesi hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu, Edson Mkasimongwa alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi saba wa upande wa mashtaka na utetezi wa washtakiwa hao anaona upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Johnson Lukaza na mdogo wake Mwesigwa Lukaza baada ya kuwaona hawana hatia katika kesi ya wizi wa  wa Sh 6.3 bilioni za akaunti ya madeni ya Nje (EPA) iliyopo Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Akitoa  hukumu hiyo  jana Kiongozi wa  jopo la Mahakimu watatu wanaoisikiliza kesi hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu, Edson Mkasimongwa alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi saba wa upande wa mashtaka na utetezi wa washtakiwa hao anaona upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka.

Mashtaka matano yaliyokuwa yakiwakabili hao ni pamoja kula njama, kughushi, kuwasilisha hati za uongo za makubaliano ya kuhamisha deni  kati ya kampuni yao ya Kernel Ltd na kampuni Marubeni ya nchini Japan na  kujipatia kiasi hicho cha fedha cha Sh 6.3 bilioni kwa njia ya udanganyifu.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mkasimongwa amesema  wamewaachia huru washtakiwa hao katika makosa hayo yote  kwa sababu ushahidi wa upande wa mashtaka haukujitosheleza kwa kuwa ulishindwa kuthibitisha kama ni kweli Novemba 2,2003 washtakiwa hao walighushi  hati  ya makubaliano ya kuhamisha deni la  Sh 6.3 bilioni baina ya kampuni  ya Kernel Ltd na Marubeni ya nchini Japan ilikuwa ni ya kughushi.

Jaji Mkasimongwa anasema ushahidi unaonesha kampuni hiyo ya Marubeni ya nchini Japan ilikubali kupokea kiasi hicho cha  fedha na kwamba  washtakiwa wao walipata  asilimia tu ya 20 ya fedha hizo na  upande wamashtaka hakuwahi kulibishia hilo.

Katika kesi hiyo, Johnson Lukaza ambaye ni  Mwenyekiti wa makampuni ya Proin na ni Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) pamoja na mdogo wake Mwesiga walikuwa wanatetewa na Wakili Alex Mgongolwa aliyekuwa akisaidiwana na Wakili Alex Mshumbusi.

Baada ya hukumu hiyo kutolewa ndugu wa washtakiwa hao waliaza kulia mahakamani hapo pamoja na mshtakiwa Mwesiga wakiwa hawa amini kilichotokea huku wakisema asante Yesu, asante Yesu.