Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mradi wa Dege wauzwa kwa mabilioni

Muonekano wa nyumba za Mradi wa Dege Eco Village uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Ikiwa ni miaka saba tangu ujenzi wake kusimama, hatimaye Mradi wa Dege Eco Village uliopo Kigamboni umepata mnunuzi.

Dar es Salaam. Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umesema hadi Oktoba 31, mwaka huu utakuwa umekamilisha hatua zote za uuzaji wa Mradi wa Dege Eco Village kwa karibu Dola 220 milioni za Marekani (zaidi ya Sh501 bilioni).

Mradi huo uliopo Kigamboni jijini hapa unapata mteja ikiwa ni baada ya ujenzi wake kusimama kwa zaidi ya miaka saba tangu Januari 2016.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba katika kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari kwa uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina kilichofanyika leo Septemba 25, 2023 jijini hapa.

Mshomba amesema Mradi huo umeuzwa kama ulivyo, ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Bodi ya Mfuko na Serikali ili kurudisha fedha za wanachama zilizowekezwa awali katika mradi huo.

Kwa mujibu wake, hadi uamuzi wa kuuzwa mradi huo unafikiwa tayari ulikuwa umeshatumia zaidi ya Sh330 bilioni huku akieleza kuwa kwa mnunuzi waliyempata watakuwa wamepata faida.

"Kwa sasa mfuko kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za Serikali unakamlisha taratibu za zabuni baada ya kukamilika kwa hatua ya tathmini ya zabuni na maafikiano ya bei. Matarajio ni kusainiwa kwa mkataba wa mauzo ya mradi huu kabla ya tarehe 31 Oktoba 2023," amesema Mshomba.

Bila kumtaja mnunuzi kutokana na taratibu kubana lakini alieleza kuwa wanaamini kuwa mnunuzi ataendelea kama ilivyokuwa imekusaudiwa.

Kwa mara ya kwanza, tangazo la kumtafuta mzabuni atakayeuendeleza mradi huo ilitangazwa Oktoba 25 mwaka jana kupitia taarifa iliyosainiwa na mkurugenzi Mshomba huku wakitaka zabuni zote kuwasilishwa kabla ya Novemba 14 mwaka huohuo.

Mradi wa Dege Eco Village wenye eneo la ekari 302, Kigamboni jijini Dar es Salaam una nyumba 3,750 zilizokuwa katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Ujenzi wake ulianza mwaka 2014 na hadi ujenzi unasimama Januari 2016 ilidaiwa kufisadi zaidi ya Sh179 bilioni ambayo ilifanya kutokamilika kwa nyumba za kifahari, hoteli, maduka makubwa, eneo la wazi la mapumziko, baa, shule, hospitali, kumbi za mikutano, nyumba za ibada na migahawa.