Mpango wa kilimo waonesha usalama wa chakula kuwa hatarini

Mabadiliko ya hali ya hewa yanatishia kushuka kwa uzalishaji wa mazao na kilimo nchini Pakistan huku serikali ikidaiwa kutochukua hatua madhubuti kumaliza tatizo hilo.
Sababu zinazotajwa kusababisha kushuka kwa kilimo cha mahindi, ngano, pamba na mpunga ni joto kali, ukame wa muda mrefu, mvua kubwa na mafuriko.
Pakistan ni miongoni mwa nchi 10 zilizoathiriwa na hali ya hewa ambapo watu zaidi ya 500 walikufa huku hasara kila mwaka ikidaiwa kuwa Dola za Marekani bilioni 3.2.
Hayo yameelezwa katika Mpango wa Kilimo Bora na Hali ya Hewa (CSA) unaoongozwa na Benki ya Dunia ukibainisha kuwa kilimo kitashuka kwa kwa kiasi kikubwa kutokana na joto kuongezeka hadi nyuzi 2.8 huku mvua ikitajw akuongezeka kwa asilimia saba hadi igikapo mwaka 2050.
"Mabadiliko ya kuongezeka kwa joto yanaweza kuleta changamoto kubwa katika kilimo hasa Kaskazini mwa Pakistan ambapo hatari ya mabadiliko ya hali ya hewa iko juu. Kuongezeka kwa joto kutaongeza mzungu