Moto wazuka kiwanda cha Yisem

Mufindi. Moto umeunguza kiwanda cha Yisem International Investment Compan Limited cha kutengeneza malighafi za mazao ya misitu katika stoo ya kuhifadhia kemikeli baada ya kutokea hitilafu wakati fundi akichomelea.
Moto huo ulizuka majira ya saa 2 asubuhi katika eneo la paa kwenye stoo ambapo fundi alikuwa akijaribu kuchomelea ambapo hadi mpaka sasa ni zaidi ya masaa 7 ambapo Jeshi la Zimamoto linaendelea na juhudi za kuuthibiti.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Dk Linda Salekwa amethibitisha kutokea kwa tukio leo Jumatatu Septemba 25, 2023 huku jitihada za kuzima moto huo zikiwa bado zinaendelea.
Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mitandao ya kijamii ya Mwananchi