Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mnyika amtaka Rais kufuta kauli Ndumbaro kuhusu katiba

Katibu Mkuu wa Chadema,John Mnyika akizungmza katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika maeneo ya Manzese jijini Dar es Salaam.

Muktasari:

  • Agosti 28, 2023 aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro alisema Serikali itatoa elimu ya mabadiliko ya katiba kwa miaka mitatu.

Dar es Salaam. Katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), John Mnyika, amemtaka Rais Samia Suluhu Hassan kujitokeza hadharani na kufuta kauli aliyowahi kuitoa aliyekuwa Waziri katiba na Sheria Dk Damas Ndumbaro kuhusu mchakato wa katiba mpya.

 Akihutubia wananchi katika mkutano hadhara wa chama hicho katika eneo la Kimara Suka leo Septemba 9, 2023 jijini hapa, Mnyika amesema hakuna haja ya elimu ya katiba kutolewa kwa miaka mitatu kwani wananchi wana uelewa na katiba.

“Rais ajitokeze ahutubie taifa aifute hiyo kauli iliyotolewa na aliyekuwa waziri wa katiba na sheria, mchakato wa katiba mpya uendelee, Watanzania wapate katiba mpya na tume huru ya uchaguzi,” amesema Mnyika.

Agosti 28, 2023 aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro alisema watatoa elimu ya mabadiliko ya katiba kwa miaka mitatu, akisema kwamba utafiti walioufanya umeonekana kuwa zaidi ya asilimia 50 ya Watanzania hawaifahamu Katiba na hata wengine hawajawahi kuiona.

Aidha Mnyika amesema Rais hapaswi kukaa kimya pindi anapoona mambo hayaendi vizuri akisema hali ngumu ya maisha kwa wananchi ikiwemo kupanda kwa gharama za maisha, si jambo la kulinyamazia.

“Rais alihutubie taifa kueleza ni hatua gani za haraka yeye kama Rais anachukua kuwaondolea wananchi mzigo mkubwa wa kupanda kwa gharama za maisha,” amesema Mnyika.