Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkandarasi ataja sababu Rea awamu ya tatu kusuasua Mtwara

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini REA, Hassan Said akizungumza katika kikao cha majadiliano ya utekelezaji wa mradi huo awamu ya tatu mzunguko wa pili mkoani Mtwara leo Jumamosi Januari 28, 2023.

Muktasari:

  • Utekelezaji wa mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili mkoani Mtwara umezorota kutokana na changamoto kadhaa zilizotajwa na wakandarasi.

Mtwara. Wakala wa Nishati Vijijini (Rea)  imesema haitatoa kazi kwa mkandarasi yeyote nchini ambaye ametekeleza mradi chini ya kiwango au kuleta usumbufu katika miradi waliyopewa.

Mkurugenzi Mkuu wa Rea, Said Hassan amesema kuwa katika tenda zinazotarajia kufunguliwa Februari 6, 2023 wakandarasi ambao hawakufikia asilimia 60 ya utekelezaji wa miradi iliyopita au inayoendelea.
"Mkandarasi ambaye anajijua alitekeleza mradi chini ya kiwango au alileta usumbufu asijisumbue kujaza makaratasi kuomba zabuni," amesema Hassan.
Mkurugenzi Mkuu amesema hayo leo wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa miradi minne ya umeme mkoani hapa ambayo imeonekana kusuasua.

Amesema Kampuni ya Central Electricals International inayotekeleza mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili katika wilaya za Mtwara Vijijini, Tandahimba na Newala wa kupeleka umeme katika vijiji 276 kwa gharama ya Sh42.7 bilioni  ameshaweka umeme katika vijiji 45 huku vingine 11 vikiwa katika hatua za mwisho.

Kampuni ya Names Corporate  Ltd inatekeleza mradi huo pia katika Wilaya za Masasi na Nanyumbu katika vijiji 124 kwa gharama ya Sh28.3 bilioni ambapo katika hivyo ni vijiji vichache ambavyo tayari vimeshawasha umeme huku vingine 18 vikitararajia kuunganishwa hivi karibuni.

Miradi mingine inayotekelezwa mkoani humu ni pamoja na kusambaza umeme katika vituo vya afya na visima vya maji na kusambaza umeme katika maeneo ya pembezoni mwa miji awamu ya tatu.

Miongoni mwa changamoto ambazo Wakandarasi hao wamezieleza kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu ni pamoja na vitendo vya hujuma hasa uchomaji wa nguzo mara tu baada ya kushushwa katika eneo la mradi.

Ugumu wa kufika kwenye maeneo ya mradi kutokana na ubovu wa barabara na baadhi ya vijiji vinapita katika mapori ya akiba hivyo kuhitaji vibali vya serikali  ili kuweza kuendelea na shughuli za mradi.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abas amewataka REA, makandarasi kukaa chini kujadili changamoto hizo ili kwa pamoja kutafuta namna ya kuzitatua hatimaye kukamilisha dhamira ya serikali ya kuweka umeme katika vijiji vyote.
Mkoa wa Mtwara una jumla ya vijiji 785 kati ya hivyo vijiji 433 vina umeme mkoani ujenzi wa mtandao w umeme katika vijiji   352 vilivyobaki vyote vipo katika mipango ya kupatiwa umeme kupitia mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza.