Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Misri yamuaga Balozi Nchimbi rasmi

Muktasari:

  • Serikali ya Misri yamuaga Balozi Emmanuel Nchimbi anayemaliza muda wake,yamshukuru kwa utendaji kazi ikiwemo kuimarisha uhusiano baina ya mataifa hayo mawili.

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Sameh Shoukry amemuaga Balozi wa Tanzania nchini humo, Dk Emmanuel Nchimbi anayemaliza muda wake huku akimshukuru kwa kazi kubwa ya kuimarisha uhusiano wa mataifa hayo.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Oktoba 3, 2023 na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imeeleza kuwa Shoukry amesema Tanzania ni moja ya nchi rafiki ya kuaminiwa na Taifa lake.

Naye, Balozi Dk Nchimbi aliyewahi kuhudumu ubalozi wa Brazili amemshukuru Waziri Shoukry na Serikali ya Misri kwa ushirikiano mkubwa waliompatia wakati akitimiza majukumu yake.

Dk Nchimbi aliyewahi kuwa mbunge wa Songea Mjini kuanzia mwaka 2005/15 sambamba na kuhudumu nafasi za uwazi katika wizara tofauti ameiomba Serikali ya Misri kumpa ushirikiano balozi mpya wa Tanzania nchini humo.

Balozi Nchimbi alianza kuiwakilisha Tanzania nchini, Misri kuanzia Machi mwaka 2022 hadi Agosti mwaka huu.

Nafasi ya Dk Nchimbi inachukuliwa na Meja Jenerali Richard Makanzo aliyehamishiwa Misri mwezi uliopita akitokea Rwanda alikokuwa akihudumu nafasi hiyo.

Balozi Nchimbi aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda kuanzia 2003/5 aliteuliwa na Rais wa awamu ya tano hayati Dk John Magufuli kuwa balozi wa Brazili Desemba 3, 2016, kabla ya Rais Samia Suluhu Hassan hajamhamishia kuhudumu Misri.


Huyu ndiye Dk Nchimbi

Alizaliwa Desemba 24, 1971 mkoani Mbeya, elimu yake ya msingi aliianizia jijini Dar es Salaam katika shule ya msingi Oysterbay kati ya mwaka 1980-1986.

Dk Nchimbi alijiunga na elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Uru kati ya mwaka 1987-1989 (kidato cha kwanza hadi cha tatu, kisha kuhamia sekondari ya Sangu kumalizia kati ya mwaka 1989-1990.

Pia Dk Nchimbi alisoma sekondari ya Forest Hill, Mbeya masomo ya kidato cha tano na sita mwaka 1991-1993. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Mzumbe (Morogoro) na kuhitimu stashahada ya juu ya utawala mwaka 1994-1997.

Wakati akihitimu masomo ya elimu ya juu, Dk Nchimbi alichaguliwa kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), na mwaka 1998 alichaguliwwa kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).

Aliwahi kuajiriwa na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kati ya mwaka 1998-2003.