Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miradi 100 ya utafiti na ubunifu kuwasilishwa

Muktasari:

  • Ni katika maadhimisho ya wiki ya 10 ya utafiti na ubunifu yatakayofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia Juni 9 hadi 11.

Dar es Salaam. Maonyesho makubwa yanatarajiwa kuonesha zaidi ya miradi 100 ya kitaaluma na ubunifu, ikiwa ni pamoja na suluhisho bunifu katika nyanja za afya, kilimo, mazingira, elimu, teknolojia ya habari, biashara, na mabadiliko ya tabianchi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm) kuanzia Juni 9 hadi 11.

Miradi hiyo ni kazi za wanafunzi na watafiti wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaama zinazolenga kutatua changamoto halisi katika jamii. Wananchi watapata nafasi ya kujifunza kwa vitendo, kushiriki mijadala, na kuona teknolojia mpya zinazoweza kubadilisha maisha yao.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Nelson Boniface amesema kufanyika kwa maonesho hayo ni mwendelezo wa kuziweka hadharani tafiti na bunifu zilizofanywa na wanataaluma wa chuo hicho na kuvuta uwekezaji katika kazi hizo.

Amesema maonyesho haya ambayo yanayofanyika kati ya Juni 9 hadi 11 yanalenga kuonesha uwezo mkubwa wa vijana wa Kitanzania katika kuibua mawazo ya kibunifu yanayoweza kubadilisha maisha ya wananchi na kuchochea maendeleo ya Taifa.

"Wanafunzi wetu pamoja na watafiti wamefanya kazi kubwa kuibua suluhisho halisi kwa changamoto zinazotukabili kila siku. Kupitia maonyesho haya, wananchi wataona kwa macho yao teknolojia na uvumbuzi wa Kitanzania unaoweza kubadilisha maisha.

“Hili limekuwa likifanyika na matunda yake yameonekana hata kwenye ripoti iliyotoka hivi karibuni inaonesha asilimia 20 ya wanaonzisha startups na kampuni ni wanafunzi waliohitimu UDSM, hawa wanakwenda pia kutoa ajira kwa wengine," alisema Profesa Boniface na kuongeza.

Ni fursa ya kipekee ndiyo maana tunawaalika wananchi kuja kushuhudia na kushiriki katika mabadiliko ya maendeleo kupitia maarifa na teknolojia. Njoo ujifunze, ushiriki na uinukie fursa mpya za kiuchumi na kijamii kupitia utafiti na ubunifu”

Amesema mara nyingi tafiti na bunifu zinaozooneshwa katika maonyesho hayo kila mwaka zinaendelezwa na zipo ambazo zinaingizwa kwenye matumizi na kuleta matokeo chanya kwenye jamii.

Mkurugenzi wa Tafiti na Bunifu,  Dk Mathew Sanga amesema katika juma hilo la utafiti mbali na maonyesho kitafanyika  kikao maalumu cha majadiliano ya ushirikiano wa kimkakati kitakachowakutanisha wadau wa elimu, viwanda, serikali na sekta binafsi kujadili namna ya kuunganisha nguvu ili kuboresha maisha ya wananchi kupitia utafiti unaotekelezeka.

“Pia kutafanyika utoaji wa tuzo kwa watafiti na wabunifu waliofanya vizuri katika nyanja mbalimbali. Lengo ni kuhamasisha ubunifu unaolenga kutoa majibu kwa changamoto za kijamii kama ajira, huduma za afya, na ustawi wa mazingira”amesema Dk Sanga.