Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikakati ya marais EAC kukabili mabadiliko tabianchi, mazingira

Muktasari:

  • Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaendelea leo Ijumaa, Novemba 24, 2023 jijini Arusha, Tanzania ambapo mikakati mbalimbali kukabili mabadiliko tabianchi.

Dar es Salaam. Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameweka msisitizo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuhifadhi mazingira kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kilimo.

Viongozi hao wamweka msimamo huo jana Alhamisi Novemba 23, 2023 jijini Arusha wakati wa mkutano wa siku mbili unaojadili masuala ya mabadiliko ya tabianchi na usalama wa chakula kwa ukanda huo.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliweka msisitizo kwa mataifa ya Afrika kuwa na vyanzo vyake vya fedha kugharamia shughuli za uhifadhi na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Alisema sasa wanakwenda kwenye mkutano wa COP28, lakini huko nyuma ahadi nyingi zilishatolewa na utekelezaji wake haujafanyika. Alisisitiza haja ya Waafrika kujitambua kwa kuangalia vyanzo vyao vya fedha za utunzaji wa mazingira.

"Nadhani ni wakati mwafaka sisi Waafrika tuache kutegemea wengine katika climate financing (kugharamia utunzaji wa mazingira). Tuje na mbinu ya kuwa na mifuko yetu ya climate financing kwa sababu tukitegemea wengine tunacheleweshwa," amesema Rais Samia

Amesema Tanzania imeanzisha mradi wa kilimo wa ''Jenga Kesho Iliyobora'' maarufu BBT kwa ajili ya wanawake na vijana, lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji wakati huohuo wakitunza mazingira.

"Kupitia programu hii, tutakuwa tunachukua hatua za kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi na pia kuzuia athari hizo ndani ya nchi yetu," amesema.

Kwa upande wake, Rais wa Kenya, Dk William Ruto alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na katika mkutano wa COP28, nchi yake itatia saini mikataba mipya ya kukabiliana na mabadiliko hayo.

"Uendelevu wa mazingira ni suala muhimu kwa kanda yetu. Kenya inapoelekea kwenye COP28, tutatia saini mkataba mpya ambao utasaidia kuongeza ukuaji wa mwamko wa tabianchi,” amesema Rais Ruto.

Naye Mwenyekiti wa EAC ambaye pia ni Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye alitaka nchi za Afrika kuwa mstari wa mbele kuandaa mikakati ya suluhisho la kushughulikia athari za mabadiliko ya tabianchi na usalama wa chakula.

Naibu Waziri Mkuu wa Uganda, Rebecca Kadaga ambaye alimwakilisha Rais Yoweri Museven, alisema: "Tunahitaji kutumia maliasili zetu na kujenga uthabiti katika mifumo yetu ya chakula. Wakati ulimwengu unatoa ahadi mpya katika mkutano wa COP28, hebu tuweke kipaumbele kutimiza ahadi zilizopita."

Waziri Mkuu wa Rwanda, Edouard Ngirente amesema: "Rwanda imejitolea kutumia kilimo kinachostahimili hali ya hewa na kusaidia kanda katika kukabiliana na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi na usalama wa chakula."