Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miili minne yapatikana ajali ya mtumbwi Katavi

Miongoni mwa miili iliyoopolewa baada ya mtumbwi kupinduka katika Mto Lunguya mkoani Katavi. Picha na Mpiga Picha Wetu

Muktasari:

  • Mtumbwi huo uliokuwa umebeba watu 14 na mizigo ulipinduka kwa kuzidiwa na uzito na kusababisha watu saba kuzama majini na wengine idadi hiyo kuokolewa.

Katavi. Miili ya watu wanne kati ya saba wanaohofiwa kufariki dunia kwa ajali ya mtumbwi katika Mto Lunguya uliopo Kitongoji cha Lunguya Kijiji cha Mwamapuli mkoani Katavi imepatikana.

Mtumbwi huo uliokuwa umebeba watu 14 na mizigo ya mazao ulipinduka Mei 26, 2024 ukidaiwa kuzidiwa na uzito na watu saba kuzama majini.

Akizungumza na Mwananchi leo Mei 27, 2024, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpimbwe, Silas Rumba akiwa kwenye eneo ilipotokea ajali hiyo amesema juhudi za kuwatafuta waliosalia zinaendelea, kwani vikosi vya uokoaji vipo vinatumia boti kutafuta miili hiyo.

"Uokoaji unaendelea hapa, mpaka sasa tayari miili ya watu wanne imepatikana kati ya saba ambao walifariki kwenye ajali hii na juhudi za kuitafuta mingine mitatu iliyobaki zinaendelea.

“Vikosi vya uokoaji vipo vinaendelea na kazi ya kuwatafuta kwa kutumia boti za kisasa, tunaamini miili iliyobaki itapatikana tu kwa uwezo wa Mungu," amesema Rumba.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwamapuli, John Alfonce amesema ajali hiyo imewasikitisha sana kwani waliopoteza maisha ni nguvu kazi iliyokuwa inatoka kwenye uzalishaji mali wakiwa na magunia 10 ya mpunga.

"Tunaomba Serikali iliangalie hili Kwa makini, kwani maji haya ni mageni kwenye hili eneo, lakini kutokana na Mto Kavuvu kuvunja kingo zake, ndio umesababisha maji hayo kuingia katika kijiji chetu na kuleta madhara kama haya,” amesema.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Inspector Lilian Wanna amesema juhudi za uokoaji zimewesesha kupatikana kwa miili minne.

“Sasa kazi ya kutafuta miili ya watu watatu bado inaendelea tunaomba wananchi waendelee kuwa na subira wakati vikosi vikiendelea kutafuta miili ya ndugu zao," amesema Wanna.