Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Michezo ya kubahatisha yachangia Sh170 bilioni kwa mwaka

Muktasari:

  • Bodi ya Michezo ya Kubahatisha itanatarajia kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake, huku ikibainisha mafanikio na mchango wake kwa mapato ya Serikali na kwa jamii kwa jumla.

Dar es Salaam. Katika kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), imeweka wazi mchango wake kwa pato la taifa ambapo umefikia Sh170 bilioni kwa mwaka.

 Pamoja na mchango huo wa kodi katika mfuko wa Serikali, pia bodi imechangia maendeleo ya jamii kwa namna tofauti tofauti, ikiwa ni pamoja na kutoa fursa za ajira katika sekta hiyo.

Haya yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, James Mbalwe, leo Jumanne, Oktoba 17, 2023, wakati akizungumzia juu ya maadhimisho hayo ya miaka 20, yanayotarajia kufanyika baadaye Oktoba 27, mwaka huu.

Mbalwe amesema kuwa malengo ya bodi hiyo kwa mujibu wa Sera ya Taifa kuhusiana na sekta ya michezo ya kubahatisha, ni kuchangia kikamilifu katika mfuko mkuu wa Serikali na kuchangia maendeleo ya jamii.

Amesema kwamba GBT imefanikiwa kufikia malengo hayo kwani mchango wa sekta hiyo umekuwa ukiongezeka kila mwaka.

“Mchango wa sekta katika mfuko mkuu wa Serikali umekuwa ukiongezeka kila mwaka. Mfamo mwaka 2006/2007 mapato ya kodi yalikuwa Sh2.8 bilioni, mapato hayo yameongezeka hadi Sh170.4 bilioni mwaka 2022/2023”, amaesema Mbalwe na kuongeza;

“Mchango wa maendeleo wa jamii kutoka kwenye sekta pia umeongezeka katika kipindi hicho kutoka fursa za ajira 600 kwa mwaka 2006/2007 hadi 25,000kwa mwaka huu wa 2022/2023.”

Mbalwe pia amesema kuwa maeneo mengine kama michezo ya kubashiri matokeo imekuwa na mchango mkubwa kwani kuanzia mwaka 2018 ilianza kuchangia asilimia 5 ya kodi itokanayo na michezo ya kubashiri.

Vilevile amesema kuwa waendeshaji na wadau walioko katika michezo ya kubashiri wamekuwa na mchango mkubwa kupitia ufadhili katika vilabu vya soka, lakini pia katika maeneo mengine ya elimu.

Kuhusu biashara, amesema kuwa bodi hiyo imekuwa na mchango katika kukuza biashara kwa kutoa vibali kwa viwanda na kampuni mbalimbali kuendesha michezo ya bahati nasibu ili kukuza biashara zao, alakini pia vibali vimetolewa kwa baadhi ya taasisi kuendesha bahati nasibu lengo likiwa kuchangia maendeleo ya jamii na katika kukuza utalii.

Mbalwe amesema kuwe kuwepo kwa sekta rasmi na pia chombo cha usimamizi yaani bodi hiyo, kumewezesha sekta ya michezo ya kubahatisha kuratibiwa na kudhibitiwa kirahisi, ili kuwalinda washiriki na kuzuia athari kwa jamii ikiwemo uwezekano wa watoto wadogo kujihusisha na michezo hiyo.

“Pia GBT imefaniwa kuweka mazingira mazuri ya uendeshaji wa sekta na kuvutia makampuni yaliyowekeza katika biashara ya michezo ya kubahatisha kutoka kampuni tisa mwaka 2003 hadi kampuni 53 mwaka 2023,” amesema Mbalwe na kuongeza:

“Pia GBT imechangia ongezeko la ubunifu kutoka katika aina hizi za michezo kutoka aina tatu ya michezo mwaka 2003 mpaka hadi kufikia zaidi ya aina Saba za michezo kuhabatisha mwaka 2023.”

Hata hivyo Mbalwe amesema kuwa changamoto wanayokabiliana nayo ni kuwepo waendeshaji haramu wa shughuli hizo za michezo ya kubahatisha, wanaochafua taswira ya sekta, lakini pia uwepo wa waendeshaji wa shughuli hizo mitanadaoni kwa njia isiyo halali.

Mwenyekiti wa Kampuni za Waendeshaji Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Sabrina Msuya amesema kuwa wanaungana na bodi hiyo katika kuhakikisha inatimiza malengo na kuhakikisha Serikali inapata mapato.

GBT ni chombo cha udhibiti wa michezo ya kubahatisha kilichoanzishwa chini ya Sheria ya Sheria ya Michezo ya Kubatisha iliyoanza kutumika Julai Mosi, 2003.

Majukumu na malengo ya bodi hiyo ni kusimamia, kufuatilia na kudhibiti uendeshaji wa shughuli za michezo ya kubahatisha nchini ili kuhakikisha uadilifu, uboreshaji wa manufaa ya muda mrefu ya kijamii na kiuchumi na ulinzi wa umma kwa kutekeleza sheria na kanuni za michezo ya kubahatisha  .