Miamala ya simu inavyozidi kuongeza tabasamu kwa watumiaji

Muktasari:
- Huduma za miamala ya simu Tanzania zimeendelea kubadilisha maisha ya watu kwa kuwapa fursa ya kutumia simu zao kufanya malipo, kutuma na kupokea pesa, kulipia huduma, na kupata mikopo midogo. Huduma hizi zimeimarika kutokana na kuongezeka kwa watumiaji wa simu za mkononi na maendeleo katika sekta ya teknolojia.
Dar es Salaam. Katika dunia ya leo, huduma za kifedha kupitia simu za mkononi zimekuwa muhimu sana kwa kila mtu ambapo Tanzania akaunti za miamala ya simu zimefikia milioni 56.
Kwa mujibu wa ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), hadi kufikia Juni 2024, kulikuwa na akaunti milioni 55.7 za pesa mtandaoni ambazo zimetumika walau mara moja ndani ya kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa akaunti za pesa mtandao ziliongezeka kwa wastani wa asilimia 1.9 kwa mwezi katika robo mwaka iliyoishia Juni 2024, huku idadi ya watoa huduma wakiwa sita (M-pesa, Tigopesa, Airtel Money, T-pesa, Halopesa na Azam Pesa).
M-Pesa ndiyo yenye akaunti nyingi zaidi (milioni 20.67), ikifuatiwa na Tigo-pesa akaunti milioni 17.82, Airtel Money akaunti milioni 11.02, Halopesa akaunti milioni 4.56, T-Pesa akaunti milioni 1.42 na Azam Pesa akaunti 187,691.
Kampuni ya Airtel Tanzania ili kuendeleza tabasamu kwa watumiaji wa huduma ya kifedha kwa simu imeleta suluhisho la kisasa kwa kuzindua kampeni ya JiBoost na Airtel Money, ambayo inalenga kuboresha maisha ya watumiaji kwa kuwapa bonasi wanapotumia huduma za Airtel Money.
Kampeni hii mpya imekuja na fursa ya kujipatia bonasi ya hadi Sh20,000 kwa kila muamala unaofanya, iwe ni kununua muda wa maongezi, malipo ya LUKU, malipo ya serikali, au hata kulipia huduma za king'amuzi.
Promosheni hiyo inawawezesha wateja
wa kawaida kuingia kwenye mfumo wa kifedha jumuishi, ambao unarahisisha malipo na kuongeza usalama wa fedha zako. Pia, inakupatia uwezo wa kudhibiti matumizi yako kupitia huduma za simu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba ameleza furaha yake kuhusu kampeni ya JiBoost na Airtel Money akisema kuwa, “Tunafurahia kuitambulisha kampeni hii ya “JiBoost na Airtel Money’ ili kuleta thamani kwa wateja wetu. Promosheni hii imetengenezwa kuwazawadia wateja wetu kila wanapotumia huduma za Airtel Money katika maisha yao ya kila siku kama manunuzi ya vifurushi vya muda wa maongezi, intaneti, au malipo ya serikali kama vile LUKU.
Naye, Balozi wa Airtel Tanzania, Nassib Abdul maarufu Diamond Platnumz ameeleza furaha yake kuhusu kampeni hiyo akusema siku zote imekuwa ikirahisisha maisha.
Kwa upande wake, Lucas Mhuvile maarufu Joti ambae alivaa uhusika wa Mr Money, amesema, “Kama Mr Money, naweza kukuambia kuwa kampeni hii ni mahususi kwa ajili ya kurudisha pesa kwenye mfuko wako.