Mganga wa kienyeji aua watoto wawili, awazika chumbani

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao. Picha na Robert Kakwesi
Muktasari:
Watoto wawili wa familia moja wameuawa na baba yao wa kambo na kisha kuwazikwa ndani ya nyumba wanayoishi.
Tabora. Watoto wawili wa familia moja wameuawa na baba yao wa kambo na kisha kuwazikwa ndani ya nyumba wanayoishi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema kuwa tukio hilo limetokea Jumatano Novemba 17, 2021 katika Kijiji na Kata ya Usimba wilayani Kaliua.
Kamanda Abwao amewataja watoto waliouawa kuwa ni Usia Yusufu (6) na Samson Yusufu (4)
"Mtuhumiwa aliwaziba midomo na pua na baada ya kuwaua kuwazika ndani ya nyumba na kukimbia" Ameeleza
Amesema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia kati yake na mkewe.
Kamanda Abwao amesema Polisi inawashikilia watu wawili kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo
Ametoa wito kwa wananchi pale wanapokuwa na migogoro kuchukua hatua za kisheria au kuonana na viongozi kwa msaada na sio kukimbilia kuchukua maamuzi ya kudhuru wengine wasiohusika.