Mfanyabiashara adaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi Morogoro

Muktasari:
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu amekiri tukio hilo kutokea.
Mfanyabiasha wa huduma za kifedha ambaye jina lake bado halijafahamika anadaiwa kuuawa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi kwa kupigwa risasi wakati akifungua duka lake kisha kuporwa begi lenye fedha usiku wa kuamkia Juni 21, 2025 huko Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu amekiri tukio hilo kutokea.
"Taarifa kamili ya tukio hilo itatolewa na Jeshi la Polisi ambao wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, baadaye atawaeleza kilichotokea," amesema Shaka.
Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Alex Mkama zinaendelea.
Endelea kufuatilia kupitia mitandao ya Mwananchi.