Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Meneja wa shule akamatwa ajali ya wanafunzi Mtwara

Muktasari:

Ajali hiyo ilitokea jana eneo la Mjimwema, Kata ya Mikindani, Mtwara Mjini na kusababisha vifo vya watu 13, kati yao ni wanafunzi 11 wa Shule ya Msingi ya King David na watu wazima wawili, akiwemo dereva wa gari hilo aina ya Toyota Hince na mwanamke mmoja aliyekuwa amepewa lifti

Mtwara. Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Shule ya Msingi ya King David, David Chibunu anashikiliwa na vyombo vya usalama kufuatia ajali ya basi iliyosababisha vifo vya watu 13 wakiwamo wanafunzi 11.

Ajali hiyo ilitokea jana Jumanne eneo la Mjimwema, Kata ya Mikindani, Mtwara Mjini na kusababisha vifo vya watu 13, kati yao ni wanafunzi 11 wa Shule ya Msingi ya King David na watu wazima wawili.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Julai 27, 2022, mmiliki wa Shule hiyo, Alex Chibunu amesema David ambaye pia ni meneja wa shule hiyo anashikiliwa na vyombo hivyo vya usalama.

“Huu kwetu ni msiba mkubwa tumepatwa na majonzi, tumeendesha shule yetu kwa miaka 19 hatujawahi kupata majonzi kama haya, wazazi wamepoteza watoto wadogo ambao tulihitaji waendelee ili wawe Taifa la kesho,” amesema na kuongeza:

“Japo sisi hatuna uwezo wa kufanya lolote zaidi ya mwenyezi Mungu kuomba atutie nguvu katika kipindi hiki kigumu kwa sasa vyombo vya usalama vinamshikilia mkurugenzi wa fedha na utawala ambaye pia ni meneja David Chibunu shule hiyo kwa upelelezi zaidi,” alisema

Katika ajali hiyo, wanafunzi watano hawakuwa wa Shule ya Msingi ya King David bali waliomba lifti ili waweze kuwahi shuleni.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikindani, Jacob Godfrey amesema wanafunzi wengi wanaosoma katika shule hiyo wanatoka maeneo ya mbali hivyo kulazimika kuomba lifti kwenye magari kutokana na changamoto ya usafiri.

Alisema katika ajali hiyo wanafunzi wake watano walikuwemo kwenye gari huku ambao ni wa shule ya sekondari Mikindani ambapo watatu wamepewa rufaa, mmoja amepelekwa Muhimbili na wawili Hospitali ya Rufaa Ndanda iliyoko wilayani Masasi.

“Kuna changamoto ya usafiri wa watoto, wanatembea umbali mrefu kufika shuleni kutokana na umbali na wamekuwa wakiomba lifti katika gari hilo na magari mengine binafsi wanapokutana nalo njiani ili kuwawahisha shuleni, tunasikitika wanafunzi wetu ni majeruhi,” alisema

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema majeruhi wanaendelea vizuri huku wengine wakipewa rufaa kwaajili ya matatibabu zaidi.

“Nimetembelea majeruhi na kuwajulia hali, majeruhi ambapo nimeona wanaendelea vizuri na matibabu na wengine wameenda kwenye uchugnuzi zaidi katika hospitlai zingine za rufaa, tuendelee kuwaombea ili warejee katika maisha yao ya kawaida,” alisema Gaguti 

Mapema leo, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Dk Clemence Haule wanafunzi saba kati ya 17 waliojeruhiwa katika ajaili hiyo wamepewa rufaa kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhumbili jijini Dar es Salaam na Hospitali ya Rufaa Ndanda, wilayani Masasi kwa matibabu zaidi huku wengine waliobaki katika hospitali hiyo wanaendelea vizuri.