Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchengerwa: Tutaendelea kutengua nafasi za uongozi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa

Muktasari:

  •  Mchengerwa atoa wiki mbili kwa uongozi wa mkoa na wilaya kuhakikisha shule ina madawati.

Simiyu. Serikali imesema itaendelea kutengua nafasi mbalimbali za uongozi kwa watendaji waliopewa dhamana  na wakashindwa kutekeleza majukumu yao, ili kuwekana sawa.

Pia imesema haitarajii kuona watendaji wakishindwa kusimamia majukumu yao katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Hayo yamesemwa jana Desemba 19,2023 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa,  alipotembelea shule ya awali na msingi Mwamashimba iliyopo wilayani Meatu, mkoani Simiyu.

Mchengerwa ametoa wiki mbili kwa uongozi wa mkoa na wilaya kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.

"Msisubiri waziri aje aseme mnunue madawati, hivi mimi nikae kule Dodoma nielekeze mnunue madawati, ninyi hamna uchungu na wananchi na watoto wanakaa chini?" amehoji Mchengerwa.

Amesema kiongozi yeyote kwenye eneo lake ambaye atakwenda kuitia aibu Serikali hadi kuandikwa kwenye magazeti na kutukanwa kwenye mitandao ya kijamii wakati viongozi wakiwapo, lazima watawachukulia hatua.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meatu, Athuman Masasi alikiri kuwapo udhaifu katika menejimenti yake, akieleza hakuna mawasiliano mazuri.

"Halmashauri haiwezi kukosa madawati 70 kwa hiyo kitu kilichotokea hapa waziri lazima niwe mkweli, ni kukosekana taarifa sahihi kutoka kwa watu wanaotusaidia kazi," amesema.

Kwa upande wa Ofisa Elimu Msingi wa halmashauri hiyo, Elizabeth Kilaya amesema taarifa za kukosekana madawati alizipata Aprili, 2023 na alitoa taarifa kwa mkurugenzi aliyepita.

"Aliniambia tuandike barua ili watendaji na jamii washiriki  kuleta maendeleo," amesema.

Amesema aliandika barua na kuipeleka kwenye shule ili kamati ishirikishwe pamoja na watendaji, pia walifanya jitihada za kutafuta wadau.