Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbowe, Lissu, Odero rasmi kuchuana uenyekiti Chadema

Muktasari:

  • Hatimaye Tundu Lissu, Freeman Mbowe na Charles Odero wameteuliwa rasmi kugombea uenyekiti wa Chadema.

Dar es Salaam. Baraza Kuu la Chadema limewateua rasmi Tundu Lissu, Freeman Mbowe na Charles Odero kuwa wagombea wa uenyekiti wa chama hicho ngazi ya taifa.

Awali, wagombea hao walichukua na kurejesha fomu za kuomba ridhaa hiyo na baadaye, Kamati Kuu iliwapitisha kuwania nafasi hiyo na uamuzi ulibaki kwa kikao cha baraza kuu.

Sambamba na wagombea wa uenyekiti, baraza kuu pia limewapitisha wagombea wa nafasi nyingine za makamu mwenyekiti bara na Zanzibar.

Wagombea wote hao, watachuana kuwania nafasi wanazoziomba katika mkutano mkuu wa Chadema unaotarajiwa kufanyika kesho ndani ya ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya uteuzi wa wagombea hao, imetolewa leo, Jumatatu Januari 20, 2025 na Mkurugenzi wa Itifaki na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema.

Amesema uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa kanuni ya 7.2.6 inayotoa ridhaa kwa vikao vya kuchuja na kuteua wagombea kuwa vya kamati za utendaji za ngazi zinazohusika na kamati kuu na baraza kuu kwa uongozi wa Kanda, kitaifa na mabaraza ya chama.

Kwa mujibu wa Mrema, walioteuliwa ni Freeman Mbowe, Odero Charles  na Tundu Lissu.

Kwa upande wa wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara, Ezekia Wenje, John Heche na Mathayo Gekul.

Kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar, walioteuliwa ni Hafidh Ali Saleh, Said Issa Mohammed, Said Mzee Said na Suleiman Makame Issa.