Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbarawa awageukia mkandarasi, Tanroads kasi ndogo ujenzi barabara

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Makame Mbarawa akikagua ujenzi wa barabara ya Tungamaa-Mkwaja-Mkange ya kilomita 95.2 ya kiwango cha lami.

Muktasari:

  • Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Makame Mbarawa amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa Barabara ya Tungamaa Mkwaja Mkange na ameagiza mkandarasi na Tanroads kuhakikisha kasi inaongezeka.

Pangani. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ameeleza kutoridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa barabara ya kutoka Tungamaa-Mkwaja-Mkange na amemuagiza mkandarasi kuhakikisha anaikamikisha haraka kwa kuwa ameshapokea kiasi kikubwa cha malipo kutoka serikalini.

Barabara hiyo ya urefu wa kilomita 95.2 ikiwamo ya kilomita 3.7 ya mchepuko wa barabara ya Kipumbwi kwa kiwango cha lami inajengwa na kampuni ya China Railway 15 Bureau Group Corporation.

Akizungumza baada ya kuikagua, Mbarawa amesema kasi yaujenzi wa barabara hiyo ni ndogo ikilinganishwa na asilimia 37 ya gharama ya ujenzi  ya Sh94.5

"Haiwezekani hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 21.96 nataka kuona kasi inaongezwa ya ujenzi ili ifikapo 2026 iwe imeshakamilika," amesema Mbarawa.

Akitoa taarifa kuhusu mradi huo, Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads), Mkoa wa Tanga, Eliazal Rweikiza amesema ulianza Januari 10, 2022 na kwa mujibu wa mkataba unatakiwa kimalizika ifikapo Januari 9 mwaka 2026.

Amesema miongoni mwa changamoto zunazochelewesha ujenzi huo ni kuchelewa kuhamisha miundombinu zikiwamo nguzo za umeme, mabomba ya majisafi, nyaya za simu na wananchi waliopisha barabara kutokubaliana na fidia ya mali zao iliyoidhinishwa na mthimini mkuu wa Serikali.

Meneja mradi wa kampuni hiyo ya ukandarasi, Zwang Yun Tao amesema ana uhakika kuwa mradi huo utatekelezwa kwa wakati kwa sababu baadhi ya mitambo ipo njiani kutoka nje ya nchi na itawasili hivi karibuni.

Amesema tayari ameweka mipango itakayowezesha ujenzi huo kukamilika kwa Wakati ikiwamo kuweka zamu za kufanya kazi usiku na mchana.

Kufuatia maelezo hayo, Waziri Mbarawa ameiagiza Tanrods na mhandisi mshauri kumsimamia ipasavyo ikiwamo kumuandikia barua za onyo kila anapochelewa ili iwe rahisi kwa Serikali kuchukua hatua kwa mkandarasi huyo atakapozembea.