Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mawakili wa Dk Slaa, Mwabukusi sasa kuishtaki Serikali

Muktasari:

  • Mawakili wanaowatetea Mwabukusi, Mdude na Dk Slaa wamefungua kesi dhidi ya Serikali wakitaka wateja wao wafikishwe mahakamani, baada ya kushikiliwa kwa wiki nzima sasa, jambo wanalosema ni kinyume cha sheria.

Dar es Salaam. Mawakili wanaotetea kina Boniface Mwabukusi, Balozi Willbrod Slaa na Mpaluka Nyagali maarufu ‘Mdude’ wapo mbioni kukamilisha taratibu za maombi ya kuzilamisha mamlaka zinazowashikilia wateja wao ikiwemo Jeshi la Polisi ziwafikishe mahakamani.

Wakili Mwabukusi na Mdude, walikamatwa Agosti 12 saa 8 usiku mkoani Morogoro, wakiwa na Katibu wa Chadema, Kanda ya Kati, Emmanuel Masonga aliyeachiwa kwa dhamana siku hiyo asubuhi yake.

Kwa upande wa Balozi Slaa, yeye alikamatwa Agosti 13, nyumbani kwake Mbweni Dar es Salaam.

Wakiwakilishwa na mawakili Dickson Matata, Jebra Kambole na Philip Mwakilima, watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda makosa ya uchochezi.

Julai 15, mwaka huu akiwasilisha mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai, mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu, Dar es Salaam Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mkuu mstaafu, Othman Chande, alipendekeza jeshi la polisi na vyombo vingine kuwafikisha watuhumiwa mahakamani kwa mujibu wa sheria yaani saa 24.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Agosti 18, 2023 kwa niaba ya mawakili wenzake, Kambole amesema wanakilimisha taratibu hizo za kuitaka mahakama iwalazimishe mkuu wa kituo cha polisi cha Mbeya pamoja na Kamanda wa Polisi wa mkoa huo kufikishwa mahakamani haraka wateja wao.

Kambole amewataja wengine ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Mwendesha mashtaka mkuu wa Serikali na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kwa pamoja wawafikishe mahakamani Mdude, Mwabukusi na Balozi Slaa.

“Tumetumia njia hii kwa sababu, wateja wetu wanashikiliwa kinyume cha utaratibu zinazoeleza kuwa muda wa kukaa nao kituo cha polisi zimepita.Tumekamilisha kwa njia ya mtandao, bado kupata kesi namba na tarehe ya kesi kutajwa na kupangiwa jaji,” amesema Kambole.

Wakili Mwabukusi, Balozi Slaa na Mdude walikamatwa siku chache tangu Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Camillius Wambura kutoa onyo kwa watu waliopanga maandamano ya kuiangusha Serikali kabla ya mwaka 2025, akiwataka wasijaribu kutingisha kiberiti.

IGP Wambura alisema kundi hilo linatumia maandamano hayo na kushawishi Watanzania kuwaunga mkono na hoja zinazoendelea za mkataba wa uwekezaji baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai (IGA).

“Mmoja amekwenda mbali zaidi na kusema watahakikisha wanaiangusha Selikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kabla ya mwaka 2025. Nimewaita hapa kuwaambia wakome kabisa na kusitisha matamshi yao ya kichochezi na tutawachukulia hatua za kisheria,” alisisitiza IGP.