Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maumivu ya moto Kariakoo, mapya yamwibua Chalamila

Dar es Salaam. Moto uliozuka juzi na kuteketeza maduka na vibanda kadhaa Kariakoo jijini hapa, umefichua mgogoro wa umiliki wa eneo la Mnadani, ambalo pia limeungua likiacha siri nzito juu ya biashara iliyokuwa inafanyika hapo.

 Eneo hilo linalodaiwa kuhusika na uuzwaji wa vifaa vya magari vilivyotumika, vikiwemo vinavyodaiwa vya wizi, limemwibua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akilitaka Jeshi la Polisi kuchunguza madai hayo.

Moto huo ambao chanzo chake hakijafahamika, ulianza juzi saa 12 asubuhi kwenye moja ya majengo ya Big Bon na kusambaa kwenye majengo mengine kadhaa na vibanda vya mnada huo wa vipuri vya magari.


Chalamila aunda kamati

Akizungumza na wafanyabiashara hao jana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amelitaka Jeshi la Polisi kudhibiti vitendo vya wizi wa vifaa vya magari na kwenda kuviuza katika eneo hilo maarufu Mnadani.

Alisema kuna wakati mtu anaibiwa kifaa chake anapofika na kukutia, kwenye mnada huo anaambiwa asiingie ndani.

“Jeshi la Polisi naomba mjipange vizuri kama nchi ikiwa na dola, mtu anakuja anaonyesha kifaa chake anaambiwa asiingie huko, haya ni mambo ya ajabu,” alisema Chalamila.

Akizungumza madhara ya moto Chalamila amesema tayari ameunda kamati itakayofanya kazi kwa siku saba itayohusisha vyombo mbalimbali ikiwemo Shirika la Umeme (Tanesco) pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama.

Mkuu wa mkoa amezitaka taasisi za fedha kuangaalia namna gani ya kuwapa unafuu wafanyabiashara waliochukua mikopo kutokana na kipindi kigumu wanachopitia.

“Jambo lingine niko na Jeshi la Zimamoto, hapa jana wakati jengo linaungua wapo watu waliokuwa wanalalamika wamechelewa, hao siyo waliowasha moto.

“Miezi michache iliyopita tulimkamata kijana mmoja akiwa na mafuta ya petroli katika Soko la Karume baada ya kuhojiwa alisema amepewa na mama mmoja ambaye alikuwa anadaiwa benki, hii nayo inaweza kuwa sababu,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo alisema tukio la moto lililotokea jana si la kwanza lakini linaenda kuwa fundisho.

Mpogolo mbali na kuvishukuru vyombo vya ulinzi na usalama pamoja kwa kazi viliyofanya kuhakikisha ulinzi na usalama, amepiga marufuku wafanyabiashara wanaotembea na majiko ya moto Kariakoo kucha.

“Kwa wale wanaotumia utaratibu huo waakikishe wanaatafuta sehemu ya kupikia au kuja na vyakula vyo kwenye vyombo, tumeshaanza vikao na wadau mbalimbali,” alisema.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kariakoo Action Mart (Mnadani) Salehe Msoka alisema moto ulianzia kwenye gorofa lililopo jirani na eneo lao, ambapo waliwasha jenereta na baada ya umeme kurudi pakalipuka.

“Watu lazima watasema moto umeanzia chini kwa sababu moto ulivyotoka juu ukahamia chini na kuonekana chanzo kimetokea kwetu,” alisema Msoka.

Kwa upande wake mmoja wa wanahisa katika mnada huo, Deus Ngamba alisema wanahisa (Mnadani) wapo 500 ambao wanajitegemea na yeye akiwa miongoni mwao, ameunguliwa na vibanda vitano.

“Viongozi wetu walipaswa kukuonyesha mkuu wa mkoa wananchi tulivyoathirika, sisi tunanunua mali na kuuza hatuwezi kupeleka fedha benki,” alisema Ngamba.


Mgogoro wa uongozi

Mapema jana akizungumza na Mwananchi, Mwenyekiti mstaafu wa Kariakoo Action Mart, Siasa Mohamed alisema katika eneo hilo kulikuwa kunafanyika shughuli mbalimbali, ikiwemo uuzaji wa vipuri ambavyo wauazaji huvipata kutoka maeneo tofauti.

Licha ya tukio hilo kuwaathiri wanahisa 500 wa eneo hilo, Mohamed alisema wapo wafanyabiashara wengine wengi walioathirika.

“Eneo hili lipo tangu mwaka 1975, uongozi umekuwa ukichaguliwa kila baada ya miaka mitatu na mimi nikiwa mmoja wa viongozi niliyedumu kwa vipindi viwili mwaka 2000 hadi 2006, nilifanikiwa kujenga maduka saba na ofisi,” alisema.

Alisema baada ya hapo wailingia viongozi wengine katika uchaguzi uliofanyika, ambao hawataki uchaguzi mwingne ufanyike.

“Chakushangaza wamefikia wakati hawataki uchaguzi, tumeenda sehemu nyingi kuwashtaki na wao wenyewe wamefika hatua ya kutukataa kuwa hii ni kampuni, sio watu 500, hadi mahakamani tumefka.


Usalama Kariakoo

Akizungumza na gazeti la The Citizen jana mtaalamu wa mipango miji kutoka Chuo cha Ardhi Morogoro, Colman Charles alisema moto ni janga kubwa duniani linalokadiriwa kuua watu 180,000.

Alitaja sababu za kukithiri kwa matukio hayo kuwa ni pamoja na mipangilio duni ya miundombimu kama majengo, barabara na mazoea ya ujenzi yasiyozingatia tahadhari.

“Katika mataifa yaliyoendelea, mbinu zinazotumika kudhibiti moto ni pamoja kutunga sheria na kanuni za ujenzi wa majengo na miundombinu mingine zinazozingatia kudhibiti moto; kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa mpango wa usalama wa moto katika majengo na ukaguzi wakati ujenzi.

Kwa Dar es Salaam na miji mingine ya Tanzania lipo jambo moja la kufikirisha. Kasi ya kuhamia mijini imekuwa kubwa kuliko kasi ya upangaji na upimaji ardhi.

“Hii inasababisha makazi holela yasiyozingatia udhibiti wa moto na athari zake,” alisema.

Ili kudhibiti hatari ya moto katika makazi, biashara na huduma, alisema lazima kuzingatia ujenzi wa majengo na miundombinu kulingana na viwango vinavyotolewa na wataalamu vya usanifu.

“Kikubwa cha kuzingatia ni kuwa ujenzi wa majengo yaliyopo katika makazi haupaswi kuongeza jumla ya mzigo wa moto uliopo wa jengo au makazi.

Ili kupunguza hatari za moto ni muhimu kufanya mabadiliko fulani ya majengo ya biashara ambayo ni hatari kwa ajili ya usalama wao na mali zao,” alisema.

Alieleza pia umuhimu wa kuzingatia umbali kati ya jengo na lingine ili kuzuia kuenea kwa moto kutoka kwa jengo moja hadi lingine la karibu.

Kanuni mojawapo ni ile inayohusiana na umbali kati ya majengo mawili yanayopakana uwe mita 12 kwa majengo ya kawaida, kwa jengo la ghorofa nne mita 16, kwa majengo ya ghorofa nane mita 22.