Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matokeo kidato cha sita 2023 haya hapa

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Said Mohamed akitangaza matokeo ya kidato cha sita na ualimu. Picha na Jesse Mikofu

Unguja. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) imetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2023 huku yakionyesha ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.26 ikilinganishwa na mwaka jana.

Akitangaza matokeo hayo leo Alhamisi Julai 13, 2023 katika ofisi za Baraza hilo Zanzibar, Katibu Mtendaji wa Necta Dk Said Mohamed amesema jumla ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani ni 106, 883 huku wasichana wakiwa ni 47, 340 na wavulana 59, 543.

"Jumla ya watahiniwa 104,549 sawa na asilimia 99.23 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha sita 2023 wamefaulu," amesema.

Wasichana waliofaulu ni 46,707 sawa na asilimia 99.51 huku kwa upande wa wavulana, waliofaulu ni 57, 843 sawa na asilimia 99.

Mwaka 2022 waliofaulu walikuwa 93,136 sawa na asilimia 98.97 hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.26 ikilinganishwa na mwaka 2023.