Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mataifa 22 wajadili kukabiliana na ujangili wa wanyamapori

Naibu Katibu Mkuu Maliasili na utalii, Benedict Wakulyamba akizungumza na wataalam pamoja na watafiti wa wanyamapori kutoka mataifa 22 katika mkutano wa nane wa Kimataifa wa mtandao wa uchunguzi wa kisayansi wa uhalifu wa wanyamapori katika bara la Afrika unaofanyika katika chuo cha Usimamizi wa wanyamapori, Mweka.Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

  •  Mkutano huo wa nane wa kimataifa unahusisha mtandao wa uchunguzi wa kisayansi wa uhalifu wa wanyamapori katika Bara la Afrika (African wildlife forensics Network), unafanyika katika chuo cha usimamizi wa wanyamapori (Mweka), Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Moshi. Wataalam na watafiti wa wanyamapori kutoka nataifa zaidi ya 22 duniani wamekutana mkoani Kilimanjaro kupeana mbinu za kutumia utaalam wa uchunguzi wa kisayansi katika kukabiliana na vita dhidi ya uhalifu wa uwindaji haramu wa wanyamapori unaotumia mtandao wa teknolojia.

Wataalam hao wamekutana jana Novemba 9 katika mkutano wa nane wa kimataifa wa mtandao wa uchunguzi wa kisayansi wa uhalifu wa wanyamapori katika bara la Afrika (African wildlife forensics Network) unaofanyika katika chuo cha usimamizi wa wanyamapori(Mweka), wilaya ya Moshi mkoani hapa.

Akizungumza katika Mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu Maliasili na Utalii, Benedict Wakulyamba amesema idara za maliasili zinahitaji kujengewa uwezo wa kutosha katika maeneo ya uchunguzi kwa kuwa wahalifu wengi wamekuwa wakitumia teknolojia za kisasa.

"Idara zetu za Maliasili zinahitaji kujengewa uwezo katika maeneo ya uchunguzi, sasa hivi wahalifu wengi wanafanya makosa kwa njia za keknolojia ya hali ya juu na hivyo tunahitaji wachunguzi wetu wanaofanya chunguzi za matukio haya kuwa na taaluma za kutosha hasa katika uchunguzi wa kisayansi.

"Kwenye kesi za uhalifu katika hifadhi zetu hali sio mbaya na matukio ya ujangili yamepungua kwa sehemu kubwa kutokana na namna vikosi vyetu vinavyofanya kazi, matukio machache yanayotokea yanachunguzwa na kesi zinaenda vizuri mahakamani," amesema.

Amesema mkutano huo utatoa fursa mbalimbali katika kujengeana uwezo wa namna ya kufanya upelelezi na kuendesha mashitaka na kwamba ndio idara muhimu katika kukamilisha mchakato wa haki jinai.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Usimamaizi wa Wanyamapori cha Mweka,  Profesa Jaffary Kideghesho amesema kama chuo watanufaika na mkutano huo na kwamba utawasadia kuboresha mitaala yao hasa katika masomo yanayohusiana na sheria ikiwa ni pamoja na kuanzisha programu ya teknolojia ya uhifadhi wa wanyamapori.

"Hapa tuna mataifa 22 yanashiriki mkutano huu ambao ni wanachama wa mtandao huu wa uchunguzi wa kisayansi wa wanyamapori katika bara la Afrika na chuo kimenufaika sana kuwa katika huu mtandao, kwa namna ambavyo walimu wetu wamepata mafunzo ya namna bora ya kufanya uchunguzi wa uhalifu wa wanyamapori," amesema.

Naye Mkemia mwandamizi kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali nchini, Leticia Waitara amesema mkutano huo utawasaidia kuongeza elimu mbalimbali katika kujadili kitaalamu sehemu ambazo zinachangamoto hasa katika kukabiliana na vita dhidi ya uhalifu wa wanyamapori.

"Kwenye uchukuaji wa sampuli za wanyamapori pamekuwa na maendeleo makubwa sana, sampuli tunazopokea katika maabara yetu huwa zinakidhi uchunguzi wa kimaabara na pale zinapokua hazikidhi huwa tunahusika katika kuelimisha wachukuaji wa sampuli kwa lengo zima la kuboresha utendaji," amesema.