Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maofisa 155 wa Polisi waliopandishwa vyeo wala kiapo

Picha ya pamoja baada ya hafla ya uapisho wa Manaibu Kamishna wa Polisi (DCPs) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACPs) leo Februari 19, 2024 baada ya kupandishwa vyeo na Rais Samia Suluhu Hassan. Picha kwa hisani ya Polisi.

Muktasari:

  • Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camillus Wambura asema wananchi watarajie mabadiliko makubwa kiutendaji.

Dar es Salaam. Maofisa wa Jeshi la Polisi 155 waliopandishwa vyeo na Rais Samia Suluhu Hassan, wamekula kiapo cha utii kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi na kiapo cha maadili ya viongozi wa umma.

 Maofisa hao ambao ni makamishna wasaidizi waandamizi wa Polisi, wapo 27 waliopanda vyeo kuwa manaibu kamishna.

Pia wamo makamishna wasaidizi wa Polisi ambao wamekuwa makamishna wasaidizi waandamizi wa Polisi, ambao ni 128.

Akitoa nasaha leo Februari 19, 2024 Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camillus Wambura amesema, kupandishwa vyeo kwa maofisa hao, kutaongeza chachu ya utendaji kazi, kutenda haki, uadilifu na nidhamu pia wananchi wategemee mabadiliko makubwa ya kiutendaji.

Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, CP Susan Kaganda amesema miongoni mwa waliopandishwa vyeo, wapo maofisa wanane wa kike, ambao wamepanda vyeo na kuwa manaibu kamishna wa Polisi.

Akizungumza kwa niaba ya waliopandishwa vyeo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi David Misime amesema kupanda kwao vyeo, kutaongeza morali na utimamu zaidi wa akili katika kutekeleza majukumu ya kazi za Polisi.